Jozi (tunda)

(Elekezwa kutoka Kokwa)

Jozi, koko au kokwa ni mbegu kavu za mimea kadhaa zinazoliwa kama chakula cha kibinadamu. Kibotania mbegu huitwa jozi kama tunda lina mbegu moja tu (mbili kwa nadra) ndani yake na ganda linalozunguka mbegu yenyewe linakauka kuwa ngumu kama ubao. Kwa lugha ya kila siku jozi inaweza kuwa pia mbegu ya tunda lenye nyama, k.m. lozi, au vitembwe, k.m. nazi (usumba).

Jozi iliyofunguliwa

Jozi na koko ni mbegu bila ganda lake, lakini kokwa kirasmi ni ganda la mbegu, ingawa watu wengi hutumia kokwa kwa maana ya mbegu pamoja na ganda lake.

Ganda la jozi kwa maana ya kibotania limeundwa kwa ukuta wa ovari. Ganda la jozi nyingine imeundwa kwa tabaka la ndani la ukuta huo (endokarpi).

Jozi ni chakula bora kwa sababu ina mafuta na protini ndani yake pamoja na vitamini na madini mbalimbali.

Mifano ya jozi

hariri
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jozi (tunda) kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Viungo vya Nje

hariri