'Kona ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2015 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Salim Ahmed (Gabo), Riyama Ally na Christian Komba. Filamu imeongozwa na Gabo na kutayarishwa na Christian Komba huku picha ikipigwa na Landline Production. Filamu ilitengenezwa mwaka 2014 huko wilayani Songea katika mkoa wa Ruvuma na kusambazwa na Steps Entertainment kwa Tanzania nzima. Muswaada andishi umeandikwa na Patrick Komba. Filamu inaelezea umuhimu wa malezi ya pande zote mbili za wazazi ili kusimamia elimu imara kwa mtoto.[1][2]

Kona
KonaFilamu.jpg
Posta ya Kona
Imeongozwa na Salim Ahmed
Imetayarishwa na Christian Komba
Imetungwa na Salim Ahmed
Nyota Ahmed Salim
Riyama Ally
Christian Komba
Imesambazwa na Steps Entertainment
Imetolewa tar. 30 Mei, 2015
Nchi Tanzania
Lugha Kiswahili

HadithiEdit

Kijana Zazuba aliyekuwa anaishi na mjomba wake, hakuwa na kipato kikubwa lakini malengo yake yalikuwa mwanaye asome hadi Chuo Kikuu. Kwa mujibu wa sheria mtoto huyo iliamriwa akae na mama yake. Mtoto huyo anakosa uangalizi mzuri katika masomo yake na umakini katika malezi maana muda mwingi bibi na mama yake wana shughuli nyingi za biashara ya pombe. Siku moja mtoto anakunywa pombe ya gongo iliyoachwa na mlevi, mwishowe anapoteza maisha kwa ungalizi mdogo.

WashirikiEdit

MarejeoEdit

  1. Mahojiano ya Gabo juu ya Kona katika Bongo Movies wavuti
  2. Kona katika watuvi ya Archived 13 Juni 2018 at the Wayback Machine. Hivi Sasa