Mapatano ya msingi ya UM kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Mapatano ya msingi ya UM kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (en:United Nations Framework Convention on Climate Change, kifupi: UNFCCC) ni mapatano ya kimataifa yaliyoanzishwa mwaka 1993. Yanalenga kupunguza kupanda kwa halijoto duniani. Njia kuu ni kuzuia ongezeko la gesi ya dioksidi kabonia

Nchi wanachama ya Mapatano ya msingi ya UM kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.

Nchi 194 zilipatana kuchukua hatua za kupunguza hatari za mabadiliko ya tabianchi. Nchi wanachama hukutana kila mwaka kujadiliana na kupatana kuhusu hatua maalumu za kufikia shabaha hizo.

Matokeo ya mikutano hii ni Miniti za Kyoto na Mapatano ya Paris kuhusu Tabianchi ambako nchi ziliahidiana kuchukua hatua maalum ya kupakana kupanda kwa halijoto duniani kwa kiwango chini ya sentigredi mbili kulingana na wakati kabla ya mapinduzi ya viwandani (karne ya 19).

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri