Krotamitoni, yaani Crotamiton, inayouzwa chini ya jina la chapa Eurax miongoni mwa zingine, hutumiwa kutibu upele, chawa, na kuwasha.[1] Kwa ajili ya matibabu ya upele, inaonekana kufanya kazi kidogo ikilinganishwa na dawa ya permetrin.[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na upele na athari za mzio.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Utaratibu wa utendakazi wake haujulikani.[1]

Krotamitoni imeidhinishwa nchini Marekani kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu tangu angalau 1949.[1] Nchini Uingereza, gramu 100 za krimu ya dawa hii hugharimu Huduma za Kitaifa za Afya (NHS) takriban £4.[2] Nchini Marekani, gramu 60 zinagharimu takriban Dola 500.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Crotamiton Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Juni 2019. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1309. ISBN 978-0857114105.
  3. "Crotamiton Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Krotamitoni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.