LA Youth
LA Youth ni gazeti la vijana kwa vijana wa Los Angeles na huchapishwa kila mwezi. Husambazwa kwa zaidi ya vituo 1,400 kama vile shule (za umma na za kibinafsi), maktaba na mashirika ya vijana.
LA Youth | |
---|---|
Jina la gazeti | LA Youth |
Aina ya gazeti | *. Gazeti la vijana kwa vijana *. Gazeti la kila mwezi |
Eneo la kuchapishwa | Los Angeles |
Nchi | Marekani |
Makao Makuu ya kampuni | Fairfax, Los Angeles |
Tovuti | http://www.layouth.com/ |
Wanafunzi wa shule ya upili (wa madarasa ya madaraja 9 - 12) ndio huwa waandishi wa habari na huhusika katika uchapishaji wa toleo la kila mwezi. Wanafunzi wa darasa la daraja la nane ,pia, wanaweza kushiriki kama kuhudhuria mikutano ya wafanyikazi, shirikiana na wengine na kuchangia katika kuchapisha jarida hili.
Waandishi huandaa kila toleo kwa kuhudhuria mikutano ya wafanyikazi ya Jumamosi, inayofanywa katika ofisi za LA Youth katika Wilaya ya Fairfax. Katika mikutano hii, waandishi wanakutana na watu wazima wanaofanya kazi nao na ,pia, wanafunzi wageni. Waandishi na wanafunzi wengine huhimizwa kuleta marafiki zao na ndugu zao ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaohusika na gazeti hili na ,vilevile, ili sauti za 'vijana wa L.A.' zisikike.
Kila mkutano huhusisha kila mwandishi/mwanafunzi kuzungumza kwa wengine wote akisema shule anayosomea, yeye hufanya nini kujifurahisha na mipango yake ya chuo kikuu ni ipi. Wanafunzi katika mikutano huwa wametoka shule tofautitofauti na miji tofauti, kama vile San Fernando Valley,Los Angeles Magharibi , Los Angeles ya ndani, na Los Angeles Mashariki. Utofauti huu wa wanafunzi unawezesha kila mwanafunzi kuwa na maoni tofauti kuhusu masuala kama mahitaji ya kuhitimu shuleni, makosa ya polisi katka utekelezaji wa kazi yao, uhalifu, vurugu na habari mbalimbali za utata.
Kila mada inayojadiliwa katika mikutano ya wafanyakazi hutumika kama mbinu ya kujulisha/kufanya mipango/kufikiria mbele. Watu wazima ambao ni wafayikazi huwapa motisha wafanyikazi vijana wakihakikisha kuwa vijana hawa wanafanya bidii na wanajifunza haraka.
Baada ya mawasilisho ya wanafunzi katika mkutano, watu wazima huchukua usimamizi kwa kuuliza kama makala yaliyokuwa yakiandikwa ama yakirekebishwa kama yamemalizwa. Iwapo mfanyikazi yeyote alikuwa anasumbuliwa na masuala, yeye anaweza kuyawasilisha kwa wafanyikazi wenzake na kupata msaada. Kuwasilisha huku kwa shida / masuala yao kunaweza kumpa mwandishi mwengine mawazo ambayo anaweza kuyaandika kama makala. Watu wazima wakikubali kuwa suala hilo ni muhimu kujadili basi mwandishi anaweza kuanza kuendeleza mawazo yake,kutafuta waandishi wengine wanaotaka kujihusisha na kisha aandike makala hayo. Waandishi wana mbinu tofauti zakuandikakatika jarida hili. Wanaweza kuandika makala katika toni binafsi, toni ripoti, na hata kuchapisha kura za maoni na maneno yaliyosemwa na watu. Wanafunzi wenye talanta ya upigaji picha na talanta ya sanaa huweza kuchangia makala kwa kupiga picha zinazohusu mada hiyo au kuchora michoro inayohusika pia.
Makala mengi ya LA Youth ni kuhusu vitu vilivyomfanyikia mtu binafsi, huweza kusaidia vijana wengine kujua jinsi ya kushughulikia shida za maisha; kuna makala ya kueleza vitendo bora vya kufanya shuleni. Kwa mfano: katika makala ya toleo la Mei - Juni 2007, mwandishi kijana ,Fred kutoka Shule ya Upili ya Birmingham katika Van Nuys, anaeleza aibu iliyompata aliposhiriki katika udanganyifu katika mitihani.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- LA Youth - Tovuti Rasmi
- LA Youth Network services Ilihifadhiwa 9 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.
- Wafanyikazi wa LA Youth