Biografia (kutoka Kiing. Biography) ni neno la kutaja hadithi ya kweli ya maisha ya mtu. Asili ya neno ni Kigiriki, hasa lilitaja bios (= maisha) na graphein (= andika). Biografia kwa Kiswahili kilichozoeleka ni "Wasifu", japo kumekuwa na tabia ya kukopa maneno. Wasifu ukiandikwa na muhusika unaitwa "tawasifu" ambapo kwa Kiingereza wanaita autobiography.