Lango:Hip hop/Makala iliyochaguliwa
Muziki wa hip hop ni aina ya muziki ulioanza kunako miaka ya 1970, ukiwa umeanzishwa na Wamarekani Weusi katika miji mikubwa ya Marekani. Hip hop mara nyingi inatumia staili moja ya kuimba iitwayo kurap au kufokafoka.
Kurap ni staili ya uimbaji ambayo mwimbaji anatoa au anaimba maneno-mashairi yaambatanayo na vina. Mashairi mengi yaliyoimbwa katika muziki wa hip hop yalikuwa yakizungumzia maisha halisi ya watu weusi wa nchini Marekani, sanasana katika miji mikubwa.
Kuna baadhi ya mashairi ya muziki wa hip hop yanazungumzia wahuni, uharifu, na utumiaji haramu wa madawa ya kulevya. Muziki wa hip hop pia huchukua tabia (mwenendo) wa staili za muziki wa pop, yaani kama disko na reggae.