Lauren Weinstein (mhandisi)
Lauren Weinstein, [1] ni mwanaharakati na mwanahabari wa nchini Marekani anayehusika na mambo ya tekinolojia ya mtandao tangu siku zake za kwanza.
Alitajwa na media mbalimbali kama mtaalamu wa maswala ya mtandao na tekinolojia[2].
Alianza kujihusisha na tekinolojia ya mtandao aliposhiriki kwenye ARPANET iliyopatikana UCLA na kuwa kitangulizi cha intaneti. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa People For Internet Responsibility (PFIR)[3] na kati ya waanzilishi wa URIICA — the Union for Representative International Internet Cooperation and Analysis.
Weinstein ameandika maoni yake kwa ajili ya jarida la Wired News akiwa pia mchambuzi wa NPR (National Public Radio) katika kipindi cha "Morning Edition". Anachangia pia kwenye sehemu ya "Inside Risks" ya jarida la Communications of the ACM [4]. Anaandika pia blogu yake. [5].
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-12-28. Iliwekwa mnamo 2022-07-26.
- ↑ Gustin, Sam (2013-06-11), "Google: We're No NSA Stooge and We'll Prove It if the Feds Let Us", Time (kwa American English), ISSN 0040-781X, iliwekwa mnamo 2022-07-26
- ↑ Privacy error (pfir.org)
- ↑ "Microsoft Academic Search", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-27, iliwekwa mnamo 2022-07-26
- ↑ "Lauren Weinstein's Blog" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-26.