Lelystad
Lelystad ni mji nchini Uholanzi na makao makuu ya mkoa wa Flevoland. Mji una wakazi 71,000.
Lelystad ni mji mpya ulioanzishwa mwaka 1967 na kama Flevoland yote ilijengwa kwenye "polder" yaani juu ya ardhi iliyowahi kuwa tako la bahari. Uholanzi uliongeza nchi kavu kwa kujenga malambo ndani ya bahari na kuondoa maji nyuma yake. Lelystad iko takriban mita 5 chini ya uwiano wa bahari.