Lemboreksanti
Lemboreksanti (lemborexant), inayouzwa kwa jina la chapa Dayvigo, ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya kulala.[1] Inaweza kutumika kwa matatizo ya kulala au kukaa usingizini.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi usingizi.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uratibu duni, kupooza wakati wa kulala au wa wakati wa kuamka usingizini, kutembea kwa usingizini, matumizi mabaya na kujiua.[1][2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni kizuizi cha vipokezi vya orexini (orexin).[1]
Lemboreksanti iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2019.[1] Nchini Marekani inagharimu takriban dola 320 kwa mwezi kufikia 2021.[4] Nchini Marekani ni dutu inayodhibitiwa na Ratiba IV.[2]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Dayvigo- lemborexant tablet, film coated". DailyMed. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "Lemborexant Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Lemborexant (Dayvigo) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dayvigo Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lemboreksanti kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |