Lesinurad, inayouzwa kwa jina la chapa Zurampic, ni dawa inayotumika kutibu asidi ya mkojo ya juu inayohusishwa na jongo.[2] Inapendekezwa kutumika tu na allopurinol au febuxostat wakati dawa hizi hazitoshi.[2] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[2]

Jina la Utaratibu la (IUPAC)
2-{[5-Bromo-4-(4-cyclopropyl-1-naphthyl)-4H-1,2,4-triazol-3-yl]sulfanyl}acetic acid
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Zurampic
AHFS/Drugs.com Kigezo:Drugs.com
MedlinePlus a616015
Taarifa za leseni EMA:[[[:Kigezo:EMA-EPAR]] Link]US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito ?
Hali ya kisheria -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo (tablets)
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili ~100%[1]
Kufunga kwa protini >98%
Kimetaboliki Ini (CYP2C9)
Nusu uhai Takriban masaa matano
Utoaji wa uchafu Mkojo (63%), kinyesi (32%)
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula C17H14BrN3O2S 

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, matatizo ya figo, na ugonjwa sugu wa njia ya juu ya utumbo ambapo yaliyomo tumboni hutiririka mara kwa mara hadi kwenye umio (GERD).[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya moyo na kiharusi.[2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Inafanya kazi kwa kuzuia URAT1 (protini inayohusaidia mwili kunyonya tena asidi ya mkojo) na OAT4 (protini inayofanana na URAT1 inayohusaidia mwili kunyonya tena asidi ya mkojo).[2]

Lesinurad iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2015.[2] Ingawa iliidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2016, idhini hii iliondolewa.[4] Haijakuwa ikipatikana tena kibiashara nchini Marekani kufikia mwaka 2021.[5]

Marejeo

hariri
  1. "Zurampic (lesinurad) Tablets, for Oral Use. Full Prescribing Information" (PDF). AstraZeneca AB, S-151 85 Sodertalje, Sweden. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 24 Desemba 2015. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Lesinurad Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Lesinurad (Zurampic) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Zurampic". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Zurampic Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)