Letermovir, inayouzwa kwa jina la chapa Prevymis, ni dawa ya kuzuia virusi inayotumika kuzuia uanzishaji upya wa cytomegalovirus (CMV) kufuatia upandikizaji wa seli za shina za alojeni.[1] Inatumika kwa wale ambao wamepatikana na kingamwili inayoonyesha wameambukizwa na CMV.[1] Dawa hii inaweza kuchukuliwa kwa mdomo au sindano kwenye mshipa.[2]

Letermovir
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
{(4S)-8-Fluoro-2-[4-(3-methoxyphenyl)-1-piperazinyl]-3-[2-methoxy-5-(trifluoromethyl)phenyl]-3,4-dihydro-4-quinazolinyl}acetic acid
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Prevymis
AHFS/Drugs.com Kigezo:Drugs.com
MedlinePlus a618006
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito B3(AU) ?(US)
Hali ya kisheria ? (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo, kwa mishipa
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 37% (takriban)
Kufunga kwa protini 98.2%
Kimetaboliki Glukuronidishaji (UGT1A1/1A3) kwa kiwango kidogo
Nusu uhai Masaa kumi na mbili
Utoaji wa uchafu 93.3% kupitia kinyesi, <2% kupitia figo
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe AIC246; MK-8228
Data ya kikemikali
Fomyula C29H28F4N4O4 

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kuhara na kutapika.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uvimbe, kikohozi, maumivu ya kichwa na uchovu.[2] Dawa hii ni kizuizi cha mchanganyiko wa DNA terminase ya virusi vya cytomegalovirus.[1]

Letermovir iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017 na Ulaya mwaka wa 2018.[2][3] Nchini Uingereza, iligharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £7,500 kwa wiki nne kufikia mwaka wa 2021.[1] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 6,200 za Marekani.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 679. ISBN 978-0857114105.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Letermovir Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Prevymis". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Julai 2021. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Prevymis Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Mei 2024. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)