Life in a Year

Life in a Year ni filamu ya mchezo wa kuigiza wa kimapenzi ya Marekani iliyoigizwa mwaka 2020 na kuongozwa na Mitja Okorn.

Nyota wa filamu hii ni Jaden Smith na Cara Derevigne. Filamu hii ilitangazwa tarehe 27 Novemba.

HabariEdit

Dyrn, ambaye alijipamba kwa Baba yake Xavier kuingia Harvard,alikutana na Isabela pindi alipokuwa anajaribu kuingia kwenye mashindano ya wanamuziki na ndipo alizama kwenye hisia za mapenzi juu ya msichana huyo. Alijaribu kuwa karibu zaidi na msichana huyo ,hatimaye alipata nafasi hiyo na alipojaribu kumueleza aligundua kuwa msichana huyo Isabela alikuwa na saratani na hakuwa na muda mwingi wa kuishi. Ndipo Dyrn alipanga kuishi ndani ya mwaka. Aliendelea kuwa karibu na Isabela na ndipo Isabela alipogundua siri ya Dyrn kuwa alikuwa na kipaji cha kuimba hivyo Isabela alimsaidia Dyrn kutoa kasiti moja ya nyimbo.Mapenzi yao yalikuwa na vikwazo vingi kikwazo kikubwa alikuwa Baba yake Dyrn ambaye alitaka mwanae haitimu kimasomo ya elimu ya juu. Kikwazo kingine kilikuwa mama yake Isabela ambaye alimterekeza Isabela akiwa na umri mdogo na kwenda kua nzisha Familia nyingine.Mwisho wa yote Dyrn na Isabela walifunga ndoa, lakini Isabela alichukua siku chache na alifariki kwa ugonjwa wa saratani. Baada ya muda mfupi Dyrn alikubaliana na baba yake kwenda mji wa New York kwa ajili ya kazi ya muziki baada ya kuhitimu masomo.

  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Life in a Year kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.