Lodoksamidi (Lodoxamide), inayouzwa kwa jina la chapa Alomide miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu mzio wa utando unaofunika sehemu nyeupe ya jicho.[1] Dawa hii iinatumika kama tone la jicho.[2] Inaweza kutumika kwa watoto zaidi ya miaka miwili.[2]

Madhara yake ya kawaida yanaweza kujumuisha kuhisi usumbufu kwenye macho na macho kavu.[2][1] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaonekana kuwa salama lakini matumizi hayo hayajafanyiwa utafiti vizuri.[3] Ni kiimarishaji cha mast cell.[2]

Lodoksamidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1993.[2] Nchini Uingereza, chupa ya mililita kumi hugharimu NHS takriban £5 kufikia mwaka wa 2021.[1] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 175 za Kimarekani.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1206. ISBN 978-0857114105.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Lodoxamide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Lodoxamide ophthalmic (Alomide) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Lodoxamide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lodoksamidi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.