Lost
Lost ni kipindi cha Marekani kinachohusu maisha ya watu waliopata ajali ya ndege iliyokuwa inatoka mjini Sydney, Australia na kuelekea mjini Los Angeles lakini ikaangukia na kupata ajali kwenye kisiwa kilichoko Oceania. Kipindi hiki kinaonyeshwa nchini Marekani kwenye stesheni ya ABC, na pia stesheni zingine kwenye nchi kadha.
Lost | |
---|---|
Nembo ya Lost | |
Aina | Maigizo, Kutisha, Aksheni |
Imeongozwa | Jack Bender Stephen Williams na wengineo |
Nchi inayotoka | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Ina misimu | 5 |
Ina sehemu | Oahu, Hawaii (Orodha ya sehemu) |
Utayarishaji | |
Watayarishaji wakuu |
J. J. Abrams Damon Lindelof Bryan Burk Jean Higgins Jack Bender Carlton Cuse Edward Kitsis Adam Horowitz Elizabeth Sarnoff |
Sehemu | Oahu, Hawaii |
Muda | makisio ni dk. 43 |
Urushaji wa matangazo | |
Kituo | ABC |
Inarushwa na | 22 Septemba 2002 - hadi leo |
Viungo vya nje | |
Tovuti ya utayarishaji |
Kwa ajili ya kuajiri waigizaji wengi, na kurekodi filamu mjini Oahu, Hawaii, kipindi hiki kinasemekana kuwa ni cha gharama ya juu sana kwenye historia ya filamu. Ilianzishwa na Damon Lindelof, J. J. Abrams na Jeffrey Lieber na imetayarishwa na ABC Studios, Bad Robot Productions na Grass Skirt Productions. Muziki wake umeundwa na Michael Giacchino.
Kipindi hiki kinachosifika kilivutia watazamaji milioni 16 kwenye mwaka wa kwanza. Imeshinda tuzo nyingi kama Primetime Emmy Award for Outstanding Drama Series mnamo 2005[1] na tuzo la Golden Globe Award for Best Television Series - Drama|Best Drama mnamo 2006.
Wahusika wakuu
hariri- Naveen Andrews aliigiza kama Sayid Jarrah, ambaye ni askari wa kutoka nchi ya Iraq.
- Emilie de Ravin aliigiza kama Claire Littleton, mwanamke mjamzito wa kutoka Australia.
- Matthew Fox aliigiza kama Jack Shepherd, ambaye ni daktari.
- Jorge Garcia aliigiza kama Hugo Reyes, ambaye ni mshindi wa pesa zilizomletea shida.
- Josh Holloway aliigiza kama mwizi aitwaye James Ford.
- Yunjin Kim aliigiza kama Sun-Hwa Kwon, ambaye ni mwana wa mwanabiashara maarufu.
- Daniel Dae Kim aliigiza kama Jin-Soo Kwon, mumewe Sun.
- Evangeline Lilly aliigiza kama Kate Austen, ambaye ni mfungwa.
- Dominic Monaghan aliigiza kama Charlie Pace, ambaye ni mwimbaji maarufu na mtumiaji madawa ya kulevya.
- Terry O'Quinn amaye aliigiza kama John Locke.
Misimu
haririMsimu wa kwanza (2004-2005)
haririIlikuwa na vipindi 25 vilivyokuwa vikionyeshwa kila Jumatano saa mbili usiku nchini Marekani kuanzia 22 Septemba 2004. Inatueleza jinsi ndege ya Oceanic 815 ilivyopata ajali. Uhai wa waliopata ajali unahatarishwa na wanyama wa msituni, jinamizi lenye miujiza, na wenyeji wabaya wa kisiwa hiki wajulikanao kama "The Others". Wanakutana na mwanamke wa Kifaransa - Danielle Rousseau - ambaye amekwama kwa kisiwa hiki kwa muda wa miaka 16.
Msimu wa pili (2005-2006)
haririIna vipindi 24 vilivyoonyesha kila Jumatano saa tatu usiku nchini Marekani na Canasa kuanzia 21 Septemba 2005. Msimu huu unazingatia vita vya waathiriwa wa ajali ya ndege dhidi ya "The Others". Tunaelezewa chanzo cha ajali ya ndege ya Oceanic 815.
Msimu wa tatu (2006-2007)
haririIna vipindi 23 vilivyoonyeshwa kila Jumatano saa tatu usiku nchini Marekani na Canada kuanzia 4 Oktoba 2006. Vita bado vinaendelea. Hata hivyo, waathiriwa wa ajali ya ndege wanapata mawasiliano na kundi linalokuja kuwaokoa.
Msimu wa nne (2008)
haririIlikuwa na vipindi 14 tu. Inaonyesha jinsi waokoaji walivyofika kwenye kisiwa hicho. Watu sita wajulikanao kama "Oceanic Six" walipata fursa ya kutoka kwenye kisiwa hiki.
Msimu wa tano (2009)
haririIna vipindi 17 vilivyoonyeshwa kila Jumatano saa tatu jioni nchini Marekani na Canada kuanzia 21 Januari 2009. "Oceanic Six" wanaamua kurudi kwenye kisiwa kwa kutumia Ajira Airways Flight 316.
Msimu wa sita (2010)
haririIlitangazwa kuwa itaanza Jumanne, 2 Februari 2010.[2]
Tuzo
haririTuzo za Primetime Emmy Awards
hariri- J. J. Abrams alituzwa kwa Outstanding Directing For A Drama Series mnamo 2005.
- Mnamo 2007, Terry O'Quinn alishinda tuzo la Outstanding Supporting Actor – Drama Series[3]
- Mnamo 2009, Michael Emerson alishinda tuzo la Outstanding Supporting Actor In A Drama Series
Tuzo za Creative Arts Emmy Awards
hariri- Mnamo 2005, Michael Giacchino alishinda tuzo la Outstanding Music Composition For A Series (Dramatic Underscore).
Golden Globe Awards
hariri- Mnamo 2006, Lost ilishinda tuzo la Best Television Series – Drama[4]
Marejeo
hariri- ↑ 58th Primetime Emmy Award Nominees and Winners - Emmys.tv
- ↑ Natalie Abrams. "ABC Sets Lost Premiere Date", TVGuide.com. Retrieved on 2010-01-25. Archived from the original on 2010-03-27.
- ↑ "'Lost': Season 3 Episode Guide", Entertainment Weekly, 2008-02-14. Retrieved on 2008-03-03. Archived from the original on 2008-02-19.
- ↑ "Golden Globe Nominations and Winners (2006)", Hollywood Foreign Press Association. Retrieved on 2008-03-02. Archived from the original on 2008-03-09.