Lota Chukwu

Muigizaji wa kike na Mwanamitindo Nigeria

Ugwu Lotachukwu Jacinta Obianuju Amelia (maarufu kwa jina la Lota Chukwu; alizaliwa Nsukka katika jimbo la Enugu nchini Nigeria[1]) ni mwigizaji ambaye alipata umaarufu baada ya kuwa nyota kwenye tamthilia ya Jenifa's Diary akiwa na Funke Akindele, Juliana Olayode, Falz ambapo alicheza kama "Kiki",[2], Jenifa. Pia ni mpenzi wa michezo ya Yoga.[3]

Maisha ya awali hariri

Lota ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wanne katika familia yake. Wakati wa utoto wake alikulia katika mji wa Benin. Lota amesomea masuala ya kilimo katika chuo kikuu cha University of Benin .

Kazi yake hariri

Kabla ya kuanza kazi ya uigizaji, Lota alikuwa mwanamitindo na alishiriki tuzo ya kuwania mwanamke mrembo kuliko wote nchini Nigeria mwaka 2011 akiwakilisha jimbo la Yobe. [4]

Alianza kazi ya uigizaji mwaka 2011 na kujipatia umaarufu kupitia filamu ya Jenifa's Diary|Jenifa's Dairy [5].

Filamu zake hariri

Mwaka Filamu Mwongoza filamu
2020 When Life Happens Okey Ifeanyi
Deadly Instincts Yemi Morafa
The Perfect Plan Uzodinma Okpechi
Wind Chasers Uzodinma Okpechi
Spotlight Sunkanmi Adebayo
Falling Niyi Akinmolayan
Dognapped[6] Kayode Kasum
Fine Girl Uduak Isong Oguamanam
The Arbitration[7] Niyi Akinmolayan
2015-2018 Jenifa's Diary[8] Funke Akindele

Marejeo hariri