Lucas Sang (12 Februari 1961[1] - 1 Januari 2008) alikuwa mwanariadha wa Kenya aliyeshiriki katika Mashindano ya Olimpiki ya 1988 yaliyofanyika kule Seoul katika timu ya Kenya ya shindano la 4 x 400 iliyofika finali na kumaliza ya nane. Pia alishiriki katika shindano la mita 400 lakini akashindwa kufika nusu fainali[2].

Lucas Sang

Kazi yake

hariri

Sang alishiriki katika mashindano ya All- Africa Games ya 1987 jijini Nairobi, Ubingwa wa Afrika wa Riadha mnamo 1998 na Kombe la Dunia la Riadha la 1998[3]. Hatimaye alibadilisha kwenda mbio za mita 800 lakini akashindwa kuwika kwa sababu ya changamoto kutoka kwa Wakenya wengine katika mbio hizo.

Baadaye alijulikana kama pacemaker kwa Wanariadha wa Kenya na Mataifa mengine[4].

Alikuwa katika timu ya Kenya ya Majeshi ya Riadha.

Kazi Baada ya Kustaafu

hariri

Baada ya kustaafu Sang alikuwa mkulima aliyekuwa na shamba kubwa kule Moiben, Wilayaya Uasin Gishu ya Kenya[3]. Pia alikuwa mfanyabiashara akishirikiana na Moses Tanui, aliyekuwa bingwa wa Dunia katika mbio za mita 10,000[4]. Pia alikuwa akijishughulisha na Uongozi katika michezo. Hadi kifo chake, alikuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Kitaifa la Wanaolimpiki wa Kenya (NAKO)[5].

Kifo chake

hariri

Baada ya ripoti za mwanzo kuwa Sang ameuawa[4], ilidhihirika baadaye kuwa alivamiwa na kuuawa na genge lililokuwa na mawe [6] katika mji wa Eldoret Siku ya Mwaka Mpya wa 2008 akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake Kisumu wakati wa Ghasia baada ya Uchaguzi wa 2007 wa Kenya kutokana na utata katika Uchaguzi wa Rais. Baada ya kugongwa kichwani na mwamba, mwili wa Sang uliteketezwa na genge hilo, ambalo linaaminika kuwa lilimchukulia kuwa wa kabila jingine shindani.

Ripoti nyingine zinaarifu kuwa Sang aliuawa na jirani zake Wakikuyu alipoliongoza kundi la vijana wa Kikalinjin kuwashambulia. Habari hizi zilitolewa kwa tovuti ya ESPN na Mkikuyu mmoja anayedai ni mmoja wa washambuliaji na pia Mkalenjin ambaye anadai kushurutishwa kujiunga katika mashambulizi hayo.[7].

Marejeo

hariri
  1. Spreadsheet of World Athletics results (1990) including Lucas Sang's date of birth (Italian)
  2. Full Olympians: Athletics - Men's 400 m
  3. 3.0 3.1 The Standard, 3 Januari 2008: Poll violence claim former athlete Sang
  4. 4.0 4.1 4.2 Kenyan Olympic runner hacked to death The Times, 2 Januari 2008
  5. IAAF, 3 Januari 2008: Violence in Kenya claims Lucas Sang, 1988 Olympian Archived 5 Juni 2011 at the Wayback Machine.
  6. Olympic athlete stoned to death by Tim Cocks, CourierMail.com.au, 5 Januari 2008 05:27am
  7. Habari kuhusu Kifo cha Sang, kutoka ESPN.com
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lucas Sang kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.