Kislavoni cha Mashariki
(Elekezwa kutoka Lugha za Kislavoni za Mashariki)
Kislavoni cha Mashariki ni kundi la lugha za Kislavoni zinazozungumzwa katika Ulaya ya Mashariki. Ni lugha tatu za Kirusi, Kiukraine na Kibelarus. Idadi ya wasemaji wa lugha hizo ni kubwa kushinda idadi ya wasemaji wa lugha za Kislavoni za Kusini au za Magharibi.
Lugha zote tatu zilitokana katika lugha moja inayoaminiwa ilitumiwa katika Ulaya ya Mashariki mnamo mwaka 1000 / 1200 BK. Ziliachana baadaye na kukuza tabia za pekee.
Lugha zote tatu hutumia mwandiko wa Kisirili.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kislavoni cha Mashariki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |