Lulikonazoli
Lulikonazoli, yaani, Luliconazole, inayouzwa chini ya jina la chapa Luzu miongoni mwa nyinginezo, ni dawa inayotumika kutibu mguu wa mwanariadha, mwasho wa maambukizi ya fangasi kwenye eneo la kati ya tumbo na sehemu ya juu ya paja, na maambukizi ya fangasi kwenye ngozi au kichwani. [1] Dawa hii inatumika kwa eneo lililoathiriwa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwashwa na maumivu.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha upele wa ngozi unaosababishwa na kugusa dutu fulani.[2] Usalama wake katika ujauzito na wakati wa kunyonyesha hauko wazi.[1] Dawa hii ni katika dawa za ngozi za familia ya imidazole. [2]
Lulikonazoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2013.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 490 kwa mirija ya gramu 60 ya krimu kufikia 2021. [3]
Marejeleo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - LULICONAZOLE cream". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Luliconazole Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Luzu Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Septemba 2016. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)