Lusutrombopagi
Lusutrombopagi (Lusutrombopag), inayouzwa kwa jina la chapa Mulpleta miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu hali pletleti kuwa chini inayosababishwa na ugonjwa sugu wa ini.[1] Inatumika kabla ya upasuaji[2] na inachukuliwa kwa mdomo.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kichefuchefu, ugonjwa wa mishipa ya ini kutokana na kuganda kwa damu kwenye mshipa wa potali (portal vein) wa ini (portal vein thrombosis), na upele.[3] Ni agonisti ya kipokezi cha thrombopoietin ambayo huongeza idadi ya chembe za pletleti. [2] [3]
Lusutrombopagi iliidhinishwa nchini Marekani mwaka wa 2018 na Ulaya mwaka wa 2019.[1] [3] Nchini Uingereza, mzunguko wa matibabu mara kadhaa unagharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £800.[2] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban USD 8,900.[4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Lusutrombopag Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1080. ISBN 978-0857114105.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 "Mulpleo EPAR". European Medicines Agency (EMA). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mulpleta Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lusutrombopagi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |