Tofauti kati ya marekesbisho "Ibuti la Jauza"

no edit summary
[[File:Position Alpha Ori.png|thumb|right|230px|Mshale wa rangi ya pinki unaoelekeza nyota upande wa kulia yenye alama ya '''[[α]]''' unaonyesha Ibuti la Jauza (Betelgeuse) katika kundinyota ya Sayadi ([[:en:Orion (constellation)|Orion]])]]
 
'''Ibuti la Jauza''' (jina la kisayansi '''Alpha Orionis''', [[ing.]] '''''[[:en:Betelgeuse|Betelgeuse]]''''') ni [[nyota]] ya aina [[jitu nyekundu]] inayoonekana katika [[kundinyota]] [[Sayadi]] (''[[:en:Orion (constellation)|Orion]]''). Ni nyota ang'avu ya tisa kati ya nyota zote zinazoonekana angani na nyota ang'avu ya pili kwenye Sayadi (Orion). Ung'avu wake unachezacheza kati ya vipimo vya 0.2 na 1.2.<ref>Davis, Kate (AAVSO Technical Assistant, Web) 2000. Variable star of the month: Alpha Orionis. ''American Association of Variable Star Observers'' (AAVSO). [http://www.aavso.org/vsots_alphaori]</ref>
 
==Jina==
Jina la Ibuti la Jauza lilijulikana tangu karne nyingi na mabaria waliotumia nyota hii kama msaada wa kukuta njia yao bahari wakati wa usiku. Asili ya jina ni Kiarabu <big>إبط الجوزاء</big> (''ibt al jauza'') na jina hili lilipokelewa pia na wanaastronomia wa Ulaya wakati wa [[karne za kati]] na kwa matamshi ya kigeni kuwa "i-bt-al-geuza" halafu "Betelgeuze". Jina la kitaalamu la kisasa ni "Alpha Orionis" ('''[[α]]''' Orionis) kwa sababu ilionekana kuwa nyota ang'avu zaidi katika kundiyota yake.<ref>Hata hivyo Ibuti la Jauza ilipewa jina la "alfa Orionis" katika [[orodha ya Bayer]] inayomaanisha ni nyota ang'avu zaidi kushinda nyingine katika kundi la nyota; inawezekana Bayer aliiona wakati iling'aa zaidi maana ung'avu wake unachezacheza, lakini kwa kawaida Rijili Kantori (Rigel) inang'aa zaidi.</ref>.
 
==Ung'avu na umbali==
Ni nyota ang'avu ya tisa kati ya nyota zote zinazoonekana angani na nyota ang'avu ya pili kwenye Sayadi (Orion). Ung'avu wake unachezacheza kati ya vipimo vya 0.2 na 1.2.<ref>Davis, Kate (AAVSO Technical Assistant, Web) 2000. Variable star of the month: Alpha Orionis. ''American Association of Variable Star Observers'' (AAVSO). [http://www.aavso.org/vsots_alphaori]</ref>
 
Umbali wake na dunia ulikadiriwa mnamo mwaka 2008 kuwa [[miaka ya nuru]] 640<ref>Harper, Graham M. ''et al''. 2008. A new VLA-Hipparcos distance to Betelgeuse and its implications. ''The Astronomical Journal'' '''135''' (4): 1430–40. [http://iopscience.iop.org/1538-3881/135/4/1430/]</ref>
 
==Hali ya nyota==
Umri wa Ibuti la Jauza hautimizi miaka milioni 10 lakini umeendelea haraka kutokana na masi yake kubwa. <ref>Levesque E.M. 2010. The physical properties of red supergiants. ''Astronomical Society of the Pacific''. 425 Hot and Cool: Bridging Gaps in Massive Star Evolution ASP Conference Series: '''103'''. [http://arxiv.org/abs/0911.4720]</ref>