Afrika ya Mashariki ya Kijerumani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 43:
Mwaka [[1913]] [[takwimu]] ya Wajerumani ilihesabu wakazi Waafrika 7,645,000, Waasia ([[Wahindi]] na [[Waarabu]]) 14,898 na [[Wazungu]] 5,336, kati yao Wajerumani 4,107. [[Nusu]] ya wakazi wote waliishi katika eneo la [[Maziwa makubwa ya Afrika|maziwa makubwa]] ambako [[serikali]] ya kikoloni iliacha maeneo ya Rwanda (wakazi 2,000,000), Burundi (1,500,000) na [[Bukoba]] (275,000) kama [[maeneo lindwa]] chini ya watawala wa kienyeji waliosimamiwa na [[afisa mkazi]] Mjerumani.<ref>[[Kamusi ya Koloni za Kijerumani]], makala "Deutsch-Ostafrika", fungu 9. Bevölkerungsstatistik.</ref>
 
== ChanzoHistoria chaya koloni ==
Historia ya koloni iliendelea katika awamu tatu:
# vyanzo kama koloni ya kampuni binafsi (Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki) kuanzia 1885 hadi kuporomoka kwa utawala wake mnamo 1890
# koloni ya Dola la Ujerumani kuanzia 1891
# mwisho wa utawala wa Kijerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia mwaka 1916 wakati jeshi kubwa la Uingereza na Afrika Kusini lilivamia, hadi kusalimisha amri kwa jeshi la [[Schutztruppe]] kwenye Novemba 1918
 
=== Utangulizi ===
Hadi mnamo mwaka [[1880]] [[serikali]] ya [[Ujerumani]] chini ya [[chansella]] [[Otto von Bismarck]] ilikataa kuanzisha makoloni. Sehemu ya [[wafanyabiashara]] Wajerumani walidai koloni. Walisikitika kuona [[faida]] za wenzao [[Waingereza]] waliopata mara nyingi msaada kutoka kwa [[wanajeshi]] na serikali za koloni za Uingereza hasa [[Asia]]. Waliona pia faida ya [[viwanda]] vya Uingereza vilivyokuwa na [[soko]] la kulindwa katika nchi kama [[Uhindi]] kwa sababu serikali ya kikoloni ilidai [[kodi]] kali kwa [[bidhaa]] zisizotoka [[Uingereza]].