Afrika ya Mashariki ya Kijerumani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 88:
==Mkataba kati ya Zanzibar na Kampuni juu ya kofo na pwani==
[[Picha:Rupie 1 DOA 1893 mbele.JPG|300px|thumb|<small>Sarafu ya rupia 1 iliyotolewa kwa jina la "Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft" (Kampuni ya Kijerumani ya Afrika ya Mashariki); tangu 1904 zilitolewa kwa jina la koloni yenyewe bila kutaja kampuni tena</small>]]
Mapatano ya 1886 yaliwapa Wajerumani nafasi ya kuendeleza upanuzi barani nyuma ya kanda la pwani la Kizanzibari na [[mstari]] wa [[mpaka]] ulichorwa kuanzia [[mdomo]] wa [[mto Umba]] kupitia [[mlima Kilimanjaro]] hadi [[Ziwa Viktoria]]. Lakini kwa ajili ya matumizi ya kibiashara suala la [[bandari|mabandari]] bado lilibaki wazi. Hapo Peters na kampuni yake walianza kujadiliana na Sultani [[Seyyed Bargash]] (alitawala 1870 hadi 1888) kuhusu utawala wa pwani katika sehemu ya [[Tanganyika]].
 
Mnamo mwaka [[1887]] Bargash alikuwa amechoka: alitafuta [[pesa]] tu kwa ajili yake binafsi; alikuwa tayari kukodisha utawala wa kanda la pwani ya Tanganyika kwa Wajerumani. Wajerumani walidai kuongezeka haki na Bargash alikufa bila kumaliza mapatano.