Umeme wa upepo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 19:
 
Katika [[Afrika]] ni hasa [[Afrika Kusini]] iliyoanza kutumia [[chanzo]] hiki cha [[nishati]]. Nchini [[Kenya]] [[Mradi wa umeme wa upepo wa Ziwa Turkana]] ulianzishwa mwaka [[2010]] ukilenga kutoa [[megawati]] 300 baada ya kukamilika.<ref>http://laketurkanawindpower.com/ </ref>
 
==Maswali kuhusu matumizi ya nguvu ya upepo==
Matumizi ya nguvu ya upepo yanapambana na matatizo kadhaa ambayo ni mabadiliko ya upepo halafu maoni kati ya wananchi wa sehemu ambako vituo vinajengwa.
 
Upepo ni mwendo wa hewa ambao uthabiti wake hubadilikabadilika. Umeme wa upepo hivyo unazalishwa kwa wingi wakati kuna upepo una mwendo mzuri. Wakati wa dhoruba mara nyingi rafadha zinasimamishwa. Wakati wa ukimya wa upepo rafadha hazizunguki na katika hali zote mbili hakuna umeme unaozalishwa. Kama mwendo wa upepo ni mdogo hata uzalishaji ni duni.
 
Kwa hiyo hata kama uwezo wa upepo wa kuzalisha umeme ni mkubwa si rahisi kufikia uzalishaji thabiti na hii inahitaji vyanzo vingine vya umeme vinavyoweza kuongeza uzalisaji wakati upepo ni hafifu. Hapo ni hasa vituo vya umeme vinavyoendeshea kwa gesi ambavyo vinaweza kuwaka haraka vikishirikiana na vituo vya umeme wa upepo.
 
Kwa jumla mabadiliko haya yanaweza kusawazishwa kama mtandao wa umeme wa nchi una uwezo wa kusafirisha viwango vikubwa vya umeme kati ya pande zote za eneo kubwa kwa sababu hapa tofauti za upepo dhaifu na mweye nguvu zinaweza kusaidiana kufikia wastani ya kawaida. Lakini hadi sasa mitandao ya nchi nyingi kubwa bado hazitoshi kwa mahitaji haya.
 
Katika nchi kadhaa kulikuwa na upinzani wa wananchi dhidi ya ujenzi wa vituo vinavyoweza kuwa na minara mamia ya rafadha za upepo kwa sababu zinabadilisha sana uso wa eneo ambao watu waazoea.
 
== Viungo vya nje ==