Kamusi ya Tiba : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Kamusi ya Tiba''' (KyT, ing. ni kamusi iliyotolewa na TUKI inayokusanya istilahi za tiba. Inapanga istilahi kwa lugha ya Kiingereza na kuonyesha visawe...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 13:46, 13 Juni 2017

Kamusi ya Tiba (KyT, ing. ni kamusi iliyotolewa na TUKI inayokusanya istilahi za tiba. Inapanga istilahi kwa lugha ya Kiingereza na kuonyesha visawe vyake vya Kiswahili.

Kamusi hii iliandaliwa na wanaistilahi wawili wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni A.M.A. Mwita pamoja na H.J.M. Mwansoko na kuchapishwa mara ya kwanza mwaka 2003 kwa kutumia ISBN 9976 911 65 3.

Kamusi hii haipatikani kwa urahisi kwenye maduka ya vitabu nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hivyo istilahi zake hazikutumiwa katika makala za kwanza za tiba zilizotungwa katika wikipedia hii.