Tofauti kati ya marekesbisho "Maradhi ya zinaa"

152 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
 
== Magonjwa ya zinaa yanayofahamika ==
 
Kuna magonjwa ya zinaa mengi, haya ni baadhi yale yanayofahamika sana.
 
=== Klamidia ===
{{main|Klamidia}}
[[Picha:Pap smear showing clamydia in the vacuoles 500x H&E.jpg|thumb|300px|right|Vijududu vinavyosababisha klamidia.]]
Klamidia ni [[ugonjwa wa kuambukiza]] ambao husababishwa na [[bakteria]] zinazoitwa na [[sayansi]] kama ''Chlamydia trachomatis''.
[[Ugonjwa]] huo huwa hauonyeshi [[dalili]] za wazi kwa karibia [[asilimia]] 75 ya [[wanawake]] na asilimia 50 ya [[wanaume]], hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.
 
Kulingana na [[wakala]] wa [[afya]] wa [[Marekani]] ''Centers for Disease Control and Prevention'' ndiyo ya kwanza kati ya [[maradhi ya zinaa]] yanayoripotiwa zaidi nchini humo: [[wataalamu]] wamekisia kuwa karibia watu [[milioni]] [[tatu]] huambukizwa klamidia kila [[mwaka]], lakini kulingana na CDC, ni [[maambukizi]] 660,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.
 
Watu ambao hawajafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute [[tiba]] na hivyo wakaendelea kufanya [[ngono]], bila ya kujua kuwa wanaeneza [[ugonjwa]].
 
=== Kisonono ===
{{main|Kisonono}}
[[Image:Gonococcal lesion on the skin PHIL 2038 lores.jpg|thumb|left|Dalili ya ugonjwa katika ngozi.]]
Kisonono au Kisalisali ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na [[bakteria]] zinazofahamika kisayansi kama ''Neisseria gonorrhoeae''. Bakteria hizo hushambulia [[utandotelezi]] unaozunguka [[sehemu za siri]].
 
 
=== Kaswende ===
{{main|Kaswende}}
[[Picha:Tertiary syphilis head.JPG|image|thumb|200px|Mfano wa kichwa cha mtu mwenye kaswende katika hatua ya tatu.]]
 
[[Kaswende]] ni gonjwa tishio linalosababishwa na [[bakteria]] inayofahamika kama ''Treponema pallidum''.
 
 
=== Malengelenge sehemu za siri ===
 
Ugonjwa wa [[malengelenge]] katika sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya ''herpes simplex virus''(HSV). Aina nyingi za malengelenge huwa ni kutokana na aina ya pili ya HSV (''HSV type 2''). hatahivyo, maambukizi kutokana na aina ya kwanza ya HSV (''HSV type 1'') nayo yapo. Malengelenge katika sehemu za siri husababisha vivimbe vinavyouma vinavyojirudia kila mara, ingawa mara nyingi ugonjwa huwa hauonyeshi dalili kwa muda mrefu. Nchini [[Marekani]], mtu mmoja kati ya watano wenye umri wa zaidi ya miaka 12 ameathirika na HSV, na idadi kubwa ya hao waliambukizwa - karibia asilimia 90 - hawafahamu kuwa wana ugonjwa. Upimaji wa [[damu]] huweza kuonyesha uwepo wa maambukizi ya HSV, hata kama mtu bado hajaanza kuonyesha dalili. Dalili za HSV zinaweza kutibika kwa kutumia madawa ya yanayopambana na virusi kama vile ''acyclovir'', lakini HSV hawawezi kutoka katika mwili - hawatibiki.
 
=== UKIMWI ===
{{main|Ukimwi}}
 
[[UKIMWI]], Ukosefu wa Kinga Mwilini, ni matokea ya maambukizi ya [[virusi vya Ukimwi]] (VVU) - ''Human immunodeficiency virus'' (HIV). [[UKIMWI]] ni ugonjwa wa zinaa hatari na usitibika ambao hushambulia [[mfumo wa kinga ya mwili]] na kumwacha mgonjwa akiwa hana hata uwezo wa kujikinga dhidi ya maambukizi madogo. Maambukizi ya VVU haimaanishi kuwa mtu ana [[UKIMWI]]. Baadhi ya watu na maambukizi ya VVU na wasionyeshe hali ya kuumwa ile inayotambulika kama UKIMWI kwa miaka kumi au zaidi. Watabibu hutumia neno [[UKIMWI]] pale mtu anapokuwa katika hatua za mwisho, zinazotishia uhai za maambukizi ya VVU.
 
 
=== Dutu za Sehemu za Siri ===
 
[[Dutu]] huota katika [[uume]] na katika eneo la kuzunguka [[uke]] na mkunduni. Husababishwa na kundi la [[virusi]] lifahamikalo kama ''human papillomavirus'' (HPV) ambao husambazwa wakati wa [[kujamiiana]]. CDC wamekadiria kuwa kuna maambukizi mapya ya dutu milioni 5.5 nchini [[Marekani]] kila mwaka. [[Dutu za sehemu za siri]] zinaweza kutibiwa na kuondolewa kwa upasuaji mdogo. Aina fulani ya HPV ambao husababisha maambukizi katika sehemu za siri wanaweza pia kusababisha [[kansa ya mlango wa uzazi]] (''cervical cancer'').
 
=== TrichomonasiTrikomonasi ===
[[TrichomonasiTrikomonasi]] husababishwa na maambukizi ya [[protozoa]] anayefahamika kisayansi kama ''Trichomonas vaginalis''. Ugonjwa huu husababisha muwasho na karaha katika [[uke]] kwa wanawake na katika mfereji wa mkojo kwa wanaume. [[Trichomonasi]] huweza kutibiwa kwa urahisi na [[antibaotiki]]. CDC wamekadiria kuwa Waamerika milioni tano huambukizwa [[trichomonasi]]trikomonasi kila mwaka.
 
[[Trichomonasi]] husababishwa na maambukizi ya [[protozoa]] anayefahamika kisayansi kama ''Trichomonas vaginalis''. Ugonjwa huu husababisha muwasho na karaha katika [[uke]] kwa wanawake na katika mfereji wa mkojo kwa wanaume. [[Trichomonasi]] huweza kutibiwa kwa urahisi na [[antibaotiki]]. CDC wamekadiria kuwa Waamerika milioni tano huambukizwa [[trichomonasi]] kila mwaka.
 
== Kuzuia na kudhibiti maambukizi ==