Kiwanda : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
ChriKo alihamisha ukurasa wa Kiwanda hadi Kiwanda (lugha): Maana ya kwanza ya kiwanda ni "industry"
 
No edit summary
Mstari 1:
#REDIRECT<sup>Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia [[Kiwanda (lughamaana)]]</sup>
 
[[File:Wolfsburg VW-Werk.jpg|thumb|250px|Kiwanda cha [[Volkswagen]] huko [[Wolfsburg]] nchini Ujerumani]]
'''Kiwanda''' ni mahali penye majengo na mashine ambako bidhaa zinazalishwa.
 
Viwanda vilisambaa hasa kuanzia karne ya 19 wakati wa [[Mapinduzi ya viwandani]] ambako uzalishaji wa bidhaa ilihamishwa kutoka kwa karahana za mafundi kwenda taasisi kubwa zaidi ambako mashine pamoja mpangilio wa kazi ziliongeza tija ya uzalishaji.
 
Ugunduzi wa [[injini ya mvuke]] uliunda msingi kwa matumizi ya mashine katika shughuli nyingi za uzalishaji. Pamoja na hayo mashine hizi zilikuwa na gharama kubwa hivyo ulimbikizi wa rasilmali uliunda tabaka mpya ya mapebari.
 
Kuenea kwa viwanda kulisababisha mabadiliko makubwa katika jamii za dunia. Mafundi wa weledi nyingi walipoteza nafasi zao kwa sababu bidhaa zilitengenezwa sasa kwa bei nafuu na katika muda mfupi, mara nyingi pia kwa ubora mkubwa kuliko jinsi mafundi waliweza kuzitoa kwa kazi ya mkono. Lakini viwanda vimeleta pia kazi mpya na ufundi tofauti na awali.
 
Uzalishaji wa bidhaa katika viwanda umekuwa msingi muhimu kwa mchakato wa [[utandawazi]] ambako bidhaa nyingi zinazalishwa katika nchi fulani na kuuzwa kote duniani ilhali vipuli vya kutengenezea bidhaa hizi tena zinatoka katika nchi tofauti.
 
[[Jamii:Uchumi]]