Kwanza Unit : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
+HashilongaBlogu
Kiduchu
Mstari 20:
'''Kwanza Unit''' (vilevile '''KU Crew''') lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la [[muziki wa hip hop]] kutoka nchini [[Tanzania]]. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1993 kwa muunganiko wa makundi kadhaa na wasanii wa rap. Awali walikuwa wanarap kwa [[Kiingereza]], lakini baadaye wakawa wanatumia [[Kiswahili]] vilevile.
 
Wanachama waanzilishi wa Kwanza Unit ikiwa ni pamoja na makundi matatu makuu ya hip-hop kwa kipindi hiko – Villain Gangsters, Raiders Posse, na Tribe-X. Kwa mujibu wa [[Rhymson]], mwanachama mwanzilishi wa kundi la Villain Gangsters, lengo la kuanzisha Unit ilikuwa ilikuwa kuifanya Tanzania kama "taifa la hip hop." Vilevile walitazamia kuondoa vijana katika maisha ya mtaani, hasa yale ya hali duni na kuweza kujitegemea na kuondokana na hali hiyo kabisa. <ref>Zavara Mponjika, katika vijambo TV, NY Marekani. http://darslamproductions.blogspot.com/2012/05/zavara-mponjika-muanzilishi-wa-kwanza.html</ref>
 
Mpango wa Kwanza Unit ulikuwa kufuata nyayo za [[Afrika Bambaataa]], Mmarekani Mweusi aliyeanzisha hip-hop ambaye pia ndiye aliyejenga [[Universal Zulu Nation]]. Kama alivyofanya [[Afrika Bambaataa]], Kwanza Unit walitaka kuchochea maadili ya taifa. Kundi lilianzisha kama kikundi chao cha utamaduni wa Kikwanza ambao ulilenga mashabiki, wasanii na yeyote yule aliyekuwa anaunga mkono maazimio yao ndani na nje ya Tanzania. Hip-hop ilitakiwa hasa iwe kiunganishi cha taifa la Wakwanza ambalo lilikuwa na miiko yake katika maisha ikiwa ni pamoja na tamaduni, thamani, na malengo yake yenyewe. Kwanza Unit inawakilisha muundo / aina ya hip-hop ya kizalendo. Kama vile jinsi Afrika Bambaataa alivyothubutu kuchochea harakati za kupinga ubaguzi na dhulma huko nchini Marekani, Kwanza Unit walitaka kuwa "alama ya mashujaa wanaopinga dhulma". Msisitizo wao ulikuwa si tu katika kupinga ubaguzi, bali pia kutambulika na mapambano dhidi ya dhulma katika nafasi za kazi.<ref>Lemelle, Sidney J. "'Ni wapi Tunakwenda': Hip Hop Culture and the Children of Arusha." In The Vinyl Ain't Final: Hip Hop and the Globalization of Black Popular Culture, ed. by Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, 230-54. London; Ann Arbor, MI: Pluto Pres</ref>