Kaa (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
(Hakuna tofauti)

Pitio la 23:17, 16 Julai 2017

Saratani ni kundinyota ya zodiaki inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Cancer. Ni moja ya kundinyota zinazotambuliwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [1]

Nyota kuu za Saratani (Cancer) jinsi zinavyoonekana angani.
Mistari imeongezwa kwenye picha tu

Jina

Jina la Kiswahili ni Saratani latokana na Kiarabu سرطان sartan linalomaanisha kaa. Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Καρκίνος karnikos kwa maana hiyohiyo na hao walipokea tayari kundinyota hii kutoka Babeli lakini Wabebli waliiona kama alama ya kobe ya maji.

Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Saratani" limesahauliwa ikiwa kundinyota inaitwa kwa tafsiri tu "Kaa".

Mahali pake

Saratani iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Jauza (Gemini) upande wa magharibi na Asadi (Leo) upande wa mashariki.

Magimba ya angani

Saratani haina nyota angavu sana si rahisi kuiona. Nyota angavu zaidi ni Beta Cancri yenye uangavu unaoonekana wa 3.8 mag. Umbali wake na dunia ni miaka ya nuru 230. Kuna fungunyota moja inayoonekana kwa macho matupu hii ni M 44 inayoitwa pia Praesepe yenye uangavu unaoonekana wa 3.7 ikionekana kama doa dogo angavu.

Tanbihi

  1. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017

Marejeo

Viungo vya Nje

 
WikiMedia Commons