Kundinyota : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 21:
Tamaduni nyingi zilipanga nyota kwa makundi. Kuna mapokeo tofautitofauti hadi leo kati ya mapokeo ya Kimagharibi, ya Kihindi na ya Kichina.
 
Mpangilio unaotumiwa na [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] (IAUUkia) uliamuliwa mwaka 1922 kwenye msingi wa elimu ya nyota ya [[Ugiriki ya Kale]] jinsi iliyoelezwa wakati wa [[karne ya 2]] [[BK]] katika kitabu cha [[Almagest]] cha [[Klaudio Ptolemaio]] wa Misri alimotaja kundinyota 48. Ptolemaio aliandika hitimisho ya elimu ya siku zake iliyoandaliwa na wanaastronomia waliomtangulia kama [[Hipparchos wa Nikaia]] na [[Eratosthenes]]. Wagiriki wenyewe waliendeleza tu elimu ya wataalamu wa [[Babeli]] waliowahi kuorodhesha nyota na kuzipanga kwa makundi.
 
Kitabu cha Ptolemaio kilifasiriwa kwa [[Kiarabu]] katika [[karne ya 9]] wakati [[Waislamu]] walitawala sehemu kubwa za nchi zenye utamaduni wa Kigiriki na kuwa msingi kwa maendeleo ya astronomia katika ustaarabu wa Kiislamu. Kwa jumla Waislamu walipokea mpangilio wa nyota kutoka Wagiriki na kufasiri majina ya kundinyota. Kuanzia [[karne ya 12]] vitabu vya Kiarabu vilifasiriwa kwa Kilatini nahivyo kupatikana kwa mataifa ya [[Ulaya]] ambako vitabu vya Wagiriki wenyewe vilipotea. Hapo majina mengi ya Kiarabu kwa nyota mbalimbali yalipokelewa katika lugha za Ulaya.
Mstari 28:
 
Mnamo mwaka 1603 Mjerumani [[Johann Bayer]] alibuni mfumo wa kutaja nyota ambao kimsingi unaendelea kutumiwa hadi leo<ref>[http://www.ianridpath.com/startales/bayer%20southern.htm Johann Bayer’s southern star chart ]</ref>. Alipanga nyota zilizoonekana na alizojua kwa kundinyota halafu kuongeza herufi kufuatana uangavu. Kwa hiyo nyota angavu zaidi katika kundinyota ilipewa [[herufi ya Kigiriki]] [[Alfa]] ( <big>α</big>), iliyofuata kwa uangavu [[Beta]] (<big>β</big>) na kadhalika. Kama kundinyota ilikuwa na idadi kubwa kushinda idadi za herufi za alfabeti ya Kigiriki aliendelea kutumia [[herufi za Kilatini]] kama a-b-c. Mfano mashuhuri ni nyota jirani ya jua letu katika anga la nje, [[Alfa Centauri]] aliyoiona kama nyota angavu zaidi katika nyota katika kundinyota ya [[Kantarusi]] ([[:en:Centaurus]]).
[[Picha:Constellations ecliptic equirectangular plot.svg|400px|thumb|Mpangilio wa anga lote kwa kundinyota kufuatana na Delporte na IAU[[Ukia]]]]
Hali hii haikuridhisha bado kwa sababu idadi nyota zilizotambuliwa kwa kutumia darubini ilizidi kuongezeka. Hivyo iliamuliwa kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] (IAU) mwaka 1922 huko Roma kufafanua idadi ya kundinyota kuwa 88<ref>[http://www.ianridpath.com/iaulist1.htm "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922], iliangaliwa Mei 2017</ref>. Mwanaastronomia [[Eugène Delporte]] kutoka Ubelgiji alipewa kazi ya kupanga eneo lote la anga kwa makundi haya na kuchora mipaka kati yao. Tokeo la kazi yake lilikubaliwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka 1928.