Tofauti kati ya marekesbisho "Ndege wa Peponi (kundinyota)"

==Jina==
Ndege wa Peponi ni kati ya kundinyota zilizobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi [[Pieter Dirkszoon Keyser]] na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika atlasi ya nyota ya [[Petrus Plancius]].
 
Keyser alitumia jina la [[Kiholanzi]] la ''De Paradijs Voghel'' ([[Ndege wa Peponi]], wa paradiso) iliyotajwa baadaye na jina la Kigirikiki „Apus“<ref>Bayer aliiiandika kwa jina "Apis Indica" inayomaanisha Nyuki wa Uhindi lakini hapa inaonekana alikosea "apis"= nyuki kwa "avis" = ndege. Johannes Kepler aliandika tayari "Avis Indica".. Ling. Wagman, Morton (2003). Lost Stars: Lost, Missing and Troublesome Stars from the Catalogues of Johannes Bayer, Nicholas Louis de Lacaille, John Flamsteed, and Sundry Others. Blacksburg, Virginia: The McDonald & Woodward Publishing Company. pp. 30–32. ISBN 978-0-939923-78-6.</ref> yaani „bila miguu“ kwa sababu wataalamu wa Ulaya waliamini mwanzoni ya kwamba Ndege wa Peponi hawana miguu. Leo iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] <ref>[https://www.iau.org/public/themes/constellations/ The Constellations], tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017</ref>
 
==Nyota==