Tofauti kati ya marekesbisho "Wanyama wa nyumbani"

548 bytes added ,  miaka 3 iliyopita
no edit summary
[[File:Zubron2.jpg|thumb|[[ Ng'ombe]] aina ya Żubroń]], [[European bison|ng'ombe]] na mseto wa mifugo.]]
'''Wanyama wa nyumbani''' au '''wanyama-kaya''' au '''mifugo''' (kutoka [[kitenzi]] "kufuga") ni wale [[wanyama]] ambao huishi katika [[mazingira]] ambayo [[mwanadamu]] anaishi. Wanyama hao wanatunzwa kwa uangalizi wa binadamu kwa ajili ya [[ulinzi]], [[michezo]], [[kazi]], [[pambo]] na majaribio ya [[maabara]].
 
Tangu [[milenia]] kadhaa wanyama hao wamepatana na wanadamu, nao ni kama vile [[mbwa]], [[mbuzi]], [[nguruwe]], [[kondoo]], [[ng'ombe]], [[paka]], [[kuku]], [[punda]], [[bata]], [[nyuki]], [[ngamia]], [[farasi]], [[njiwa]], [[kware]] na wengine wengi.
Wanyama hao wana [[faida]] katika maisha ya wanadamu; kwa mfano ng'ombe hupatia watu [[maziwa]], [[nyama]], pia [[ngozi]] yake inaweza kutumika kutengeneea vitu mbalimbali.
 
Mbwa husaidia hasa katika suala la [[ulinzi]] katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu.
 
Mbuzi huwapatia watu nyama, maziwa ila si mazuri kama yale ya ng'ombe na pia ngozi yake hutumika kutengenezea vitu kama vile [[ngoma]], hasa katika [[jamii]] za [[Afrika]].
 
Kware ni [[Ndege (mnyama)|ndege]] mdogo; [[mayai]] yake ni madogo sana yana faida kubwa katika [[mwili]] wa mwanadamu kwa sababu yanasemekena kutibu baadhi ya [[magonjwa]] katika miili yetu.
 
Wanyama hao hutoa pia faida za kihisia kama mazoezi, mahusiano ya kijamii na n.k. Wanyama hawa huondoa upweke kwa watu wasiokuwa na marafiki au mahusiano ya kijamii kama [[wazee]], [[watoto]], [[Ujauzito|wajawazito]]. Wanyama wengine huwatembelea [[wagonjwa]].
 
Wanyama hawa hufundiswa jinsi ya kufanya vitu vya kisayansi, kwa kulenga wagonjwa.
 
Hivyo tunaweza kuona faida za wanyama hao: ni vizuri tukiwatunza vizuri kwani tunawategemea katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi.
 
1. Wanyama hawatakiwi kupigwa.
2. Wanyama wanatakiwa waangaliwe afya zao.
3. Wanyama wanatakiwa kupata mahitaji yao.
 
{{mbegu-utamaduni}}