Kundinyota : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 27:
Baada ya uenezaji wa mataifa ya Ulaya kupitia wapelelezi kama [[Kristoforo Kolumbus]], [[Vasco da Gama]] na [[Ferdinand Magellan]] wanaastronomia wa Ulaya walipokea taarifa na ramani za nyota za nusutufe ya kusini ya dunia na kuongeza kundinyota kwa nyota ambazo hazikujulikana kwao bado.
 
Mnamo mwaka 1603 Mjerumani [[Johann Bayer]] alibuni mfumo wa kutaja nyota ambao kimsingi unaendelea kutumiwa hadi leo<ref>[http://www.ianridpath.com/startales/bayer%20southern.htm Johann Bayer’s southern star chart ]</ref>. Alipanga nyota zilizoonekana na alizojua kwa kundinyota halafu kuongeza herufi kufuatana uangavu. Kwa hiyo nyota angavu zaidi katika kundinyota ilipewa [[herufi ya Kigiriki]] [[Alfa]] ( <big>α</big>), iliyofuata kwa uangavu [[Beta]] (<big>β</big>) na kadhalika. Kama kundinyota ilikuwa na idadi kubwa kushinda idadi za herufi za alfabeti ya Kigiriki aliendelea kutumia [[herufi za Kilatini]] kama a-b-c. Mfano mashuhuri ni nyota jirani ya jua letu katika anga la nje, [[Rijili KantarusiKantori]] (Alfa Centauri) aliyoiona kama nyota angavu zaidi katika nyota kwenye kundinyota ya [[Kantarusi]] ([[:en:Centaurus]]).
[[Picha:Constellations ecliptic equirectangular plot.svg|400px|thumb|Mpangilio wa anga lote kwa kundinyota kufuatana na Delporte na [[Ukia]]]]
Hali hii haikuridhisha bado kwa sababu idadi nyota zilizotambuliwa kwa kutumia darubini ilizidi kuongezeka. Hivyo iliamuliwa kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] (IAU) mwaka 1922 huko Roma kufafanua idadi ya kundinyota kuwa 88<ref>[http://www.ianridpath.com/iaulist1.htm "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922], iliangaliwa Mei 2017</ref>. Mwanaastronomia [[Eugène Delporte]] kutoka Ubelgiji alipewa kazi ya kupanga eneo lote la anga kwa makundi haya na kuchora mipaka kati yao. Tokeo la kazi yake lilikubaliwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka 1928.