Imani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Fides - Capella dei Scrovegni - Padua 2016.jpg|160px|thumb|right|Mchoro wa [[Giotto]], ''Imani'', [[Padua]]]]
{{Maadili ya Kimungu}}
Ingawa'''Imani''' kwa [[Kiswahili]] ni [[neno]] '''imani''' linalenye maana mbalimbali (k.mf. "huruma"), lakini ile kuu inahusiana na [[kitenzi]] '''kuamini''', kinachofanana na '''kusadiki'''. Hapo ni kukubali [[ukweli]] wa jambo lisiloweza kuthibitishwa.
 
Ingawa kwa [[Kiswahili]] neno '''imani''' lina maana mbalimbali (k.mf. "huruma"), ile kuu inahusiana na kitenzi '''kuamini''', kinachofanana na '''kusadiki'''. Hapo ni kukubali [[ukweli]] wa jambo lisiloweza kuthibitishwa.
 
Katika [[dini]] msingi wake ni [[mamlaka]] ya [[Mungu]] aliyeshirikishwa ukweli huo kwa njia ya [[ufunuo]] maalumu ili kumsaidia [[binadamu]] amjue yeye, ajifahamu pamoja na maisha yake [[dunia]]ni na [[ahera]].
Line 11 ⟶ 10:
 
==Roho ya imani katika [[maisha ya kiroho]]==
Kila mara [[mtu]] anafuata ama [[umbile]], asipopita fikra za kibinadamu tu, ama [[imani]], anapolenga [[mbinguni]] kwa njia ya [[utakatifu]]. Roho hizo zinazotuongoza maishani ni namna maalumu za kupima, kuona, kuhisi, kupenda, kushabikia, kutaka na kutenda. Basi, roho ya imani ni kupima yote kwa mtazamo wa juu ambao unapita maumbile na kutegemea [[mamlaka]] ya [[Mungu]] katika kujifunua, na [[ukweli]] wake katika kutushirikisha [[utukufu]]. Tunaelewa zaidi roho ya imani tukiangalia iliyo kinyume chake, yaani [[upofu wa roho]] unaozuia mtu asione mambo ya Mungu isipokuwa kidunia na kutoka nje. Hivyo [[Israeli]] haikuelewa [[uteuzi]] wake kadiri ya ukweli wa Mungu ulio wa juu kuliko [[ukabila]] au [[ubaguzi]] wowote.
 
Imani ina mitazamo mipana kuliko huo kutokana na [[usahili]] wake unaoshiriki [[hekima]] ya Mungu. Juu sana kuliko mifuatano ya mawazo, ni tendo sahili ambalo tunamsadiki Mungu anayefunua na papo hapo anajifunua. Kwa tendo hilo lipitalo maumbile tunaambatana naye pasipo [[udanganyifu]] na hivyo katika [[giza]] tunalenga kutazama mambo ya Mungu, juu kuliko [[hakika]] zote za kibinadamu. Hakika inayotokana na imani tuliyomiminiwa na Mungu, inapita hata hakika ya [[akili]] tunayoweza kujipatia kwa kuzingatia [[miujiza]] inayothibitisha [[ufunuo]] wake.
Line 24 ⟶ 23:
 
==Imani tuliyomiminiwa inatakiwa kustawi hadi kifo==
 
Imani inatakiwa kukua kila [[siku]]. “Imani inaweza ikawa kubwa ndani ya [[Ukristo|Mkristo]] mmoja kuliko ndani ya mwingine, upande wa akili kutokana na hakika na [[imara]] kubwa zaidi katika kushika ufunuo, na upande wa utashi kutokana na [[utayari]] na [[utiifu]] au [[tumaini]] kubwa zaidi” kwa kuwa “imani tunayomiminiwa inalingana na zawadi ya neema, ambayo si sawa kwa wote” ([[Thoma wa Akwino]]). [[Yesu Kristo]] aliwasema wanafunzi wake kuwa “wa imani haba” ([[Math]] 6:30); kumbe alimuambia [[mwanamke]] [[Mkananayo]], “[[Mama]], imani yako ni kubwa!” (Math 15:28).
 
Line 48 ⟶ 46:
 
Kabla ya imani yetu kutakaswa kwa majaribu kadhaa ya aina hiyo, tujitahidi kukua katika imani, badala ya kupima yote kibinadamu tu. Ni lazima tujinyime mianga midogo na ya bandia ili tujaliwe ile ya juu; tuache kufuata mno akili yetu ili tuone [[uangavu]] mkuu wa mafumbo ya imani na kuishi kulingana nayo. Hivyo tunaelewa kwa nini hatutakiwi kuitikia vishawishi dhidi ya imani, bali kuvikataa au kuviruka kwa kukiri imani kwa dhati zaidi; [[Bwana]] anaviruhusu kwa maendeleo yetu tu.
 
==Tazama pia==
*[[Imani sahihi]]
*[[Imani ya Kanisa]]
 
[[Jamii:Dini]]
Line 54 ⟶ 56:
[[Jamii:Maadili]]
[[Jamii:Maisha ya kiroho]]
 
[[cs:Víra]]
[[el:Πίστη]]
[[hr:Vjerovanje]]
[[hu:Hit (vallás)]]
[[zh:信念]]