Dhambi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 63 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q60227 (translate me)
No edit summary
Mstari 1:
'''Dhambi''' ni [[kosa]] la [[kiumbe]] mwenye [[hiari]] dhidi ya [[uadilifu]] unaompasa.
 
Inaweza kufanyika kwa mawazo, maneno, matendo na kutotimiza [[wajibu]].
 
[[Maadili]] yanamuelekeza [[binadamu]] katika kutambua dhambi ni zipi pamoja na madhara yake.
 
Kwa kawaida [[dini]] zinahusianisha kosa hilo na [[Mungu]] aliye [[asili]] ya uadilifu, kwa kuwa ndiye aliyeumba viumbe vyote na kuvielekeza [[Maisha|maishani]].
 
Akiwapa baadhi ya viumbe[[viumbehai]] [[akili]] na [[utashi]], papo hapo Mungu amewapa [[wajibu]] wa kufuata maelekezo yaliyomo katika [[utaratibu]] wa [[nafsi]] yao na wa [[ulimwengu]] wote.
 
Katika [[dini]] zinazofundisha kwamba Mungu alitoa [[ufunuo]] wake hata kwa njia ipitayo [[maumbile]], ni dhambi kwenda kinyume cha ufunuo huo, kwa mfano unavyopatikana katika [[vitabu]] vitakatifu vya dini husika, kama vile [[Biblia]] kwa [[Wayahudi]] na [[Wakristo]] na [[Kurani]] kwa [[Waislamu]].
 
Kutokana na uenezi wa dhambi kuanzia [[dhambi ya asili]], linajitokeza suala la [[wokovu]].