Ekaristi : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
No edit summary |
No edit summary |
||
Mstari 1:
[[Picha:01preparation4.jpg|thumb|200 px|right|Vipaji vya [[mkate]] na [[divai]] vilivyoandaliwa kwa [[adhimisho]] la ekaristi.]]
{{Ukristo}}
== Jina ==
[[Jina]] linatokana na [[neno]] la [[lugha]] ya [[Kigiriki]] εὐχαρίστω (''eukharisto'': "nashukuru") lililotumiwa na [[Mtume Paulo]] na [[Wainjili]] katika kusimulia [[karamu]] hiyo ya mwisho ya [[Yesu]] na [[Mitume wa Yesu|Mitume]] wake, na [[muujiza]] uliotangulia ambao [[Yesu]] alidokeza nia yake ya kushibisha [[binadamu]] wote, yaani ule wa kuzidisha [[mkate]] na [[samaki]] kwa ajili ya [[umati]].
Jina linaonyesha [[mazingira]] ya [[sala]] ya matukio hayo, ambapo Yesu alimuelekea [[Mungu]] akimshukuru kwa [[vyakula]] na [[kinywaji]] alivyoshika [[Mikono|mikononi]] kabla hajawagawia [[wanafunzi]] wake.
[[Shukrani]] ilikuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa [[mungu Baba|Baba]] [[maisha]] yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe [[kafara]] ya [[wokovu]] wa
Ndiyo [[maandishi]] ya kale zaidi tuliyonayo juu ya tukio hilo.
== Mkate na divai ==
Yesu alitumia mkate na [[divai]] kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika [[utamaduni]]
Mara nyingine [[Wakatoliki]] wanapokea [[umbo]] la mkate tu kwa lengo la kukwepa umwagaji wa [[Damu ya Kristo]] na kurahisisha [[ibada]], hasa kama washiriki ni umati (hata [[milioni]] 4 katika misa [[moja]] ilivyotokea [[Manila]] ([[Ufilipino]])). Yesu mwenyewe alizungumzia mkate kuliko divai, kwa sababu chakula ni muhimu kuliko [[kileo]]. “Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu” (Yoh 6:51). “Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja” (1Kor 10:17).
“Melkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana” ([[Mwa]] 14:18), “amefananishwa na Mwana wa Mungu” ([[Eb]] 3:7). “Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana” ([[Isa]] 25:6). “Njoo, ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya” ([[Mith]] 9:5-6). Yesu alishiriki karamu nyingi na katika mojawapo ndipo alipoanza [[Miujiza ya Yesu|miujiza yake]] kwa kugeuza [[pipa|mapipa]] ya [[maji]] kuwa divai bora. “Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa” (Yoh 2:10). “Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mwasema, ‘Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi” ([[Lk]] 7:34).
Hatimaye Yesu alitumia divai kuachia [[ishara]] ya damu yake ili wafuasi wake waweze kushiriki mateso yake. “Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?” ([[Math]] 20:22). Kisha kushiriki kila [[mwaka]] karamu ya [[Pasaka]], ambapo wote walikunywa divai mara [[nne]], safari ya mwisho alikamilisha miujiza yake kwa kuigeuza iwe damu yake. “‘Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu’. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, ‘Twaeni hiki, mgawanywe ninyi kwa ninyi; maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja’. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, ‘Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu’” (Lk 22:15-20). “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo?” (1Kor 10:16).
== Ushuhuda wa [[Biblia]] ==
[[Agano Jipya]] linasimulia mara nne matendo na maneno ya Yesu ambayo alianzisha ibada hiyo na kuwakabidhi [[Mitume wa Yesu|Mitume wake]].
Simulizi la zamani zaidi ni lile la [[Barua ya kwanza kwa Wakorintho|1Kor]] 11:23-25. Likafuata lile la [[Injili ya Marko|Mk]] 14:22-24; halafu yale ya [[Injili ya Mathayo|Math]] 26:26-28 na [[Injili ya Luka|Lk]] 22:19-20.
== Asili ==
Kadiri ya ushuhuda huo, Yesu, katika karamu ya mwisho aliwagawia mitume wake mkate na divai akisema ndio mwili wake na damu yake vitakavyotolewa kama [[kafara]] kwa ondoleo la [[dhambi]] za umati,
Hivyo [[Kanisa]] tangu hapo, linaendeleza ibada hiyo maalumu na ya msingi katika mazingira mbalimbali.
Simulizi la Paulo linafanana na lile la [[Mwinjili Luka]] na kufuata jinsi ekaristi ilivyoadhimishwa kati ya [[Wakristo wa mataifa]]; kumbe [[Mwinjili Marko]] na [[Mwinjili Mathayo]] waliripoti adhimisho lilivyokuwa kati ya [[Wakristo wa Kiyahudi]].
== Maendeleo ==
[[Picha:BentoXVI-51-11052007.jpg|thumb|left|360px|[[Papa Benedikto XVI]] akiadhimisha ekaristi]]
[[Karne]] zilizofuata ibada ilizidi kubadilika, hasa ilipotenganishwa na [[mlo]] wa kawaida ulioendana nayo awali. Badala ya mlo huo, ibada iliunganishwa na masomo ya [[Neno la Mungu]].
Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio wa kupanda: waamini wanalishwa Neno la Mungu katika [[mimbari]], halafu [[Mwili na Damu ya Kristo]] katika [[altare]]. Vilevile sehemu ya kwanza ([[liturujia ya Neno]]) inaleta masomo yakiwa na [[kilele]] katika [[Injili]]. Halafu katika sehemu ya pili ([[liturujia ya ekaristi]]) padri anafuata alichofanya Yesu katika karamu ya mwisho: anatwaa mkate na divai (kuandaa [[dhabihu
Kati ya namna mbalimbali za kuiadhimishwa, yalijitokeza [[Ukristo wa Mashariki|mapokeo ya mashariki]] na [[Ukristo wa Magharibi|ya magharibi]]. Kwa jumla mapokeo ya mashariki yanahusisha [[milango ya fahamu]] na ni ya [[fahari]] kuliko yale ya magharibi.
== Teolojia ==
Kadiri ya Injili Yesu Kristo aliweka ekaristi wakati wa kuadhimisha karamu ya [[Pasaka ya Kiyahudi]], akaipatia maana mpya kuhusiana na [[Msalaba wa Yesu|kifo]] na [[Ufufuko wa Yesu|ufufuko wake]].
[[Madhehebu]] mengi ya Kikristo yamekubali hati ya ki[[ekumeni]] ya [[Lima]] ([[1982]]) inayosema "Ekaristi ni ukumbusho wa Yesu msulubiwa na mfufuka, yaani ishara hai na ya nguvu ya sadaka yake, ambayo ilitolewa mara moja tu msalabani na inaendelea kutenda kwa faida ya binadamu wote".
Wakatoliki na [[Waorthodoksi]] wanaamini kwamba katika karamu ya Bwana wanakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi [[padri]] anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai
Baada ya [[mageuzo]] Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji
Vilevile Wakatoliki na Waorthodoksi wanaamini ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu
Ekaristi inaitwa sakramenti ya [[upendo]] kwa sababu kila unapofanyika ukumbusho wa sadaka hiyo pekee waamini wanazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1). Hivyo
== Katika mpangilio wa sakramenti saba ==
{{sakramenti}}
Katika [[imani]] ya [[Kanisa Katoliki]] na [[Waorthodoksi]] sakramenti inayokamilisha [[ubatizo]] na [[kipaimara]] ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai. Walioshiriki kifumbo kifo na ufufuko wake wakapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, wanaalikwa kukaribia mara kwa mara [[meza]] anapowalisha na kuwanywesha Mwili na Damu yake ili washiriki [[uhai]] wake kwa dhati zaidi na zaidi. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi” (Yoh 6:56-57). Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani ya mtu kama [[mifupa]] ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.
{{mbegu-Ukristo}}
Line 62 ⟶ 63:
[[Jamii:Liturujia]]
[[Jamii:Sakramenti]]
[[Jamii:Teolojia]]
|