Tofauti kati ya marekesbisho "Kitabu cha Mhubiri"

8 bytes added ,  miaka 3 iliyopita
no edit summary
'''Mhubiri''' (pia: '''Koheleti''') ni kimojawapo kati ya [[vitabu chavya hekima]] vilivyomo katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebrania]]) na hivyo pia katika [[Agano la Kale]] la [[Biblia ya Kikristo]]. Kwa sababu hiyo kilidhaniwa kimeandikwa na [[mfalme Solomoni]], kielelezo cha [[hekima]] katika [[Biblia]].
 
[[Kitabu]] hicho kina [[sura]] [[kumi na mbili]] na kwa kiasi kikubwa kimeandikwa kwa njia ya [[ushairi]].
Yeye anakabili masuala ya [[maisha]] kwa kuzingatia upande chanya na upande hasi wa kila moja ili kufikia [[hekima]].
 
Hasa anajiuliza juu ya maana ya [[maadili]] wakati [[ufunuo]] wa [[Mungu]] ulikuwa haujafikia hatua ya kufundisha [[uzima wa milele]] na maisha yalikuwa yanaonyesha mara nyingi ustawi wa waovu na hali ngumu ya waadilifu.
 
Mbele ya utovu wa [[haki]] [[duniani]], Mhubiri alikariri, "Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili" (1:2).
 
Hata hivyo, hatimaye akajumlisha mawazo yake kwa kuhimiza kwa [[imani]], "Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" (12:13-14).