Afya : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6:
Afya ya [[binadamu]] itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani [[chakula]] chenye [[virutubishi]] vyote, vikiwemo [[protini]], [[wanga]] na [[fati]] (hiyo iwe katika [[asilimia]] ndogo sana).
 
Pia anatakiwa awe msafi mwilini na mazingira yake, kama vile kwa kuoga na kusafisha mazingira yanayomzunguka. Mandhari yenye [[hewa]] safi pia husaidia katika kuhifadhi afya ya binadamu katika mwili na akili. <ref>http://www.selfgrowth.com/articles/how-to-improve-your-mind-and-body-with-fresh-air "''Jinsi ya kuimarisha mwili na akili kwa hewa safi"''</ref>
 
Mazingira mara nyingi huchukuliwa kuwa jambo muhimu katika hali ya afya ya binadamu. Hii inajumuisha mazingira ya asili, mazingira ya kujengwa, na mazingira ya kijamii. Pia mambo kama vile maji safi na hewa, makazi salama, huchangia afya nzuri, hasa kwa afya ya watoto wachanga na watoto.<ref>http://www.who.int/hia/evidence/doh/en/</ref>
 
Utafiti umeonyesha kuwa ukosefu wa maeneo ya burudani husabsabisha kupungua kwa afya na ustawi. <ref>https://doi.org/10.1136%2Fjech.2007.062414 "''Faida za maeneo ya burudani kwenye afya"''</ref>
 
Pia anatakiwa kuwa na afya ya kiroho yaani kuishi kadiri ya mafundisho ya [[Mwenyezi Mungu]] kama vile: kupendana na wengine, kuthaminiana na kuacha [[dhambi]]: mara nyingi hizo zinadhuru afya ya mwili pia.
Mstari 21:
* [[Mwanafalsafa]] [[Friedrich Nietzsche]]: "Afya ni [[kiwango]] cha ugonjwa kinachoniruhusu kutekeleza [[shughuli]] zangu muhimu."
 
* [[Mwanasosholojia]] [[Talcott Parsons]]: "Afya ni hali ya [[mtu]] kuwa na [[uwezo]] bora wa kutekeleza shughuli alizofundishwa kukubali kama [[wajibu]] wake." <ref>https://www.cliffsnotes.com/study-guides/sociology/health-and-medicine/sociological-perspective-on-health "''Makala inayomnukuu Talcott Parsons"''</ref>
 
* Kwa watu wengi ni hali ya kutosumbuliwa na [[maumivu]] na [[udhaifu]], pamoja na uwezo wa kutumia sehemu zote za mwili. Ni wazi ya kwamba [[hisia]] hii ni tofauti kati ya mtu na mtu.