Mifano ya Yesu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Tengua pitio 955320 lililoandikwa na Jocktan Thobias (Majadiliano)
No edit summary
Mstari 1:
[[File:Guercino_Return_of_the_prodigal_son.jpg|thumb|300px250px|''[[Mfano wa mwana mpotevu]]'' ulivyochorwa na [[Guercino]].]]
{{Yesu Kristo}}
'''Mifano ya Yesu''' inaweza kusomwa katika [[Injili]] zote 4[[nne]] za [[Agano Jipya]] katika [[Biblia ya Kikristo]], lakini pia katika Injili nyingine zilizoandikwa baadaye. [[Injili ya Luka]] ndiyo inayoongoza kwa wingi wa mifano (50 hivi).
 
Ni sehemu muhimu ya [[utume wa Yesu]], ikiwa sawa na [[thuluthi]] moja ya mafundisho yake yote yaliyotufikia kwa [[maandishi]].
 
[[Wakristo]] wanatia maanani sana mifano hiyo kama maneno ya [[Yesu]] yanayohitaji kufikiriwa zaidi ili kuelewa yanataka kusema nini kweli.<ref name="JDPentecost10">J. Dwight Pentecost, 1998 ''The parables of Jesus: lessons in life from the Master Teacher'' ISBN 0-8254-3458-0 page 10</ref><ref>Eric Francis Osborn, 1993 ''The emergence of Christian theology'' ISBN 0-521-43078-X page 98</ref>
 
Ni kwamba mifano ya Yesu inaonekana kwanza [[hadithi]] za kuvutia zinazochora vizuri [[maisha]] ya watu yalivyokuwa katika [[mazingira]] yake. Hata hivyo [[wataalamu]] wanaonyesha kwamba [[ujumbe]] wa dhati umefichika hasa katika sehemu ya mwisho ya habari, ambapo kuna jambo lisilo la kawaida, yaani lisilotokea kweli.<ref name="Lisco9-11">Friedrich Gustav Lisco 1850 ''The Parables of Jesus'' Daniels and Smith Publishers, Philadelphia pages 9–11</ref><ref>Ashton Oxenden, 1864 The parables of our Lord William Macintosh Publishers, London, page 6</ref>
 
Ingawa mifano inaonekana kusimulia habari za kawaida, lengo ni kufikisha ujumbe wa ki[[dini]] kwa wasikilizaji wenye nia njema, ambao wanapokea changamoto ya Yesu, "Mwenye masikio, na asikie!".
 
Mifano ya Yesu inabaki kati ya masimulizi maarufu zaidi [[duniani]] kote.<ref name="William Barclay page 9">William Barclay, 1999 ''The Parables of Jesus'' ISBN 0-664-25828-X page 9</ref>
 
Kwa [[Kiebrania]] [[neno]] husika ni מָשָׁל ''mashal'' linalodokeza pia ''[[fumbo]]'' au ''[[kitendawili]]''. [[Agano la Kale]] lilikuwa tayari na mifano ya namna hiyo, hivyo Wayahudi wa wakati wa Yesu waliweza kuelewa ya kwake kwa urahisi fulani.<ref>Pheme Perkins, 2007 ''Introduction to the synoptic gospels'' ISBN 0-8028-1770-X page 105</ref>
 
==Tanbihi==