Tofauti kati ya marekesbisho "Ufufuko"

1,444 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
no edit summary
d (Bot: Migrating 41 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q188681 (translate me))
No edit summary
[[File:Kern Vision des Ezechiel.jpg| thumb |Mchoro wa Leonhard Kern, ''Njozi ya Ezekieli'', kwenye Schwäbisch Hall.]]
'''Ufufuko''' (kutoka [[kitenzi]] "kufufua") ni hali ya [[mwili]] kurudi kuishi baada ya [[kufa]], kwa mfano wa kuamka kutoka [[usingizi|usingizini]].
 
[[Dini]] mbalimbali zinasadiki uwezekano wake, ingawa kwa misingi na mitazamo tofauti.
 
Kuna [[visasili]] kuhusu [[miungu]] kufa na kufufuka mara kwa mara, kwa mfano wa [[uhai]] wa [[uasilia]] katika mzunguko wa [[majira]], hasa katika [[majira ya kuchipua]] baada ya [[majira ya baridi]].
 
Tofauti na [[hadithi]] hizo, [[Biblia]] inafundisha [[uwezo]] wa [[Mungu]] juu ya [[kifo]] cha [[binadamu]], kwamba kupitia [[manabii]] kama [[Elia]] na [[Elisha]], yeye aliwarudishia uhai watu waliokufa tangu muda mfupi.
 
Baada ya [[nabii Ezekieli]] kupata [[njozi]] kuhusu ufufuko wa [[mifupa]] mikavu iliyozagaa bondeni, [[Wayahudi]] walizidi kukubali kwamba Mungu atafufua wafu wote.
 
[[Injili]] zinasimulia jinsi [[Yesu Kristo]] alivyofufua [[vijana]] watatu kwa nyakati tofauti: [[binti]] [[Yairo]], [[mvulana]] wa [[Nain]] na [[Lazaro wa Bethania]].
 
Lakini jambo kuu la [[vitabu]] hivyo ni kwamba mwenyewe aliweza kufufuka [[siku]] ya [[tatu]] baada ya [[Kifo cha Yesu|kufa]] [[Msalaba wa Yesu|msalabani]], tena si kwa kurudia [[maisha]] ya [[duniani]], bali kwa kuingia [[uzima wa milele]] akiwa na mwili mtukufu.
 
[[Yesu]] alitabiri kwamba atarudi kutoka huko siku ya mwisho ili afufue wafu wote na [[Hukumu ya mwisho|kuwahukumu]].
 
[[Uislamu]] pia unafundisha kwamba mwishoni kutakuwa na ufufuo wa wafu wote (Yawm al-Qiyāmah, kwa [[Kiarabu]]: يوم القيامة‎‎). Siku hiyo imepangwa na Mungu lakini haijafunuliwa kwa binadamu.
 
==Tazama pia==
 
[[Category:Dini]]
[[Jamii:Uyahudi]]
[[Category:Ukristo]]
[[Jamii:Uislamu]]