Kundinyota : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 25:
Kitabu cha Ptolemaio kilifasiriwa kwa [[Kiarabu]] katika [[karne ya 9]] wakati [[Waislamu]] walitawala sehemu kubwa za nchi zenye utamaduni wa Kigiriki na kuwa msingi kwa maendeleo ya astronomia katika ustaarabu wa Kiislamu. Kwa jumla Waislamu walipokea mpangilio wa nyota kutoka Wagiriki na kufasiri majina ya kundinyota. Kuanzia [[karne ya 12]] vitabu vya Kiarabu vilifasiriwa kwa Kilatini nahivyo kupatikana kwa mataifa ya [[Ulaya]] ambako vitabu vya Wagiriki wenyewe vilipotea. Hapo majina mengi ya Kiarabu kwa nyota mbalimbali yalipokelewa katika lugha za Ulaya.
 
Baada ya uenezaji wa mataifa ya Ulaya kupitia wapelelezi kama [[Kristoforo Kolumbus]], [[Vasco da Gama]], [[Ferdinand Magellan]] na [[Pieter DirkzoonDirkszoon Keyser]] wanaastronomia wa Ulaya walipokea taarifa na ramani za nyota za nusutufe ya kusini ya dunia na kuongeza kundinyota kwa ajili ya nyota ambazo hazikujulikana kwao bado. Hapo alikuwa hasa Mholanzi [[Petrus Plancius]] aliyebuni kundinyota mpya 12.
 
Mnamo mwaka 1603 Mjerumani [[Johann Bayer]] alibuni mfumo wa kutaja nyota ambao kimsingi unaendelea kutumiwa hadi leo<ref>[http://www.ianridpath.com/startales/bayer%20southern.htm Johann Bayer’s southern star chart ]</ref>. Alipanga nyota zilizoonekana na alizojua kwa kundinyota halafu kuongeza herufi kufuatana uangavu. Kwa hiyo nyota angavu zaidi katika kundinyota ilipewa [[herufi ya Kigiriki]] [[Alfa]] ( <big>α</big>), iliyofuata kwa uangavu [[Beta]] (<big>β</big>) na kadhalika. Kama kundinyota ilikuwa na idadi kubwa kushinda idadi za herufi za alfabeti ya Kigiriki aliendelea kutumia [[herufi za Kilatini]] kama a-b-c. Mfano mashuhuri ni nyota jirani ya jua letu katika anga la nje, [[Rijili Kantori]] (Alfa Centauri) aliyoiona kama nyota angavu zaidi katika nyota kwenye kundinyota ya [[Kantarusi]] ([[:en:Centaurus]]).