Arthur Schopenhauer : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
dNo edit summary
d +++
Mstari 41:
 
Katika maoni ya mara kwa mara ya siasa katika kazi zake za ''Parerga and Paralipomena'' na ''Manuscript Remains'', Schopenhauer anajieleza mwenyewe kama mpendekezi wa serikali finyu. Cha mno, alidhani, ni kuwa serikali inapaswa “kuwacha kila mtu huru ajitafutie wokovu wake mwenyewe”,  na ikiwa serikali itasita kudoea au kuingilia haya, yeye alipendekeza zaidi “afadhali kutawaliwa na simba kuliko panya wenzake”- hiyo nikumaanisha, na mfalme, kuliko kiongozi wa demokrasia. Schopenhauer aliunga mkono maoni ya Thomas Hobbes ya umuhimu wa serikali, na wa utendakazi wake, kuchunga mielekeo yetu ya uharibufu ambayo ni ya undani na imeambatana na asili ya aina yetu. Yeye bado alitetea tawi huru za utunga-sheria, mahakama, na utekelezaji za nguvu, na aliona mfalme kama kipengele huru ambacho kinaweza tekeleza haki (anamaanisha katika matumizi ya kila siku, sio kwa maana ya kikosmologia). Alitangaza ufalme kama “kile ambacho ni cha hali ya kawaida kwa binadamu” kwani “uerevu daima chini ya serikali ya ufalme umekua ukipata nafasi bora zaidi kupiku adui wake mkuu, ujinga” alihujumu ujamhuri kama “yasiyo asili kwani inasusia hatua za uerevu wajuu, sanaa na sayansi”
 
=== Utata wa nungunungu ===
 Utata wa nungunungu, ni fumbo wa changamoto zinazoathiri umoja na urafiki wa watu. Huelezea hali ambayo jamii ya nungunungu hujaribu kusongeana karibu pamoja ili kugawana joto katika msimu wa baridi. Lakini hupata kwamba zinaumizana na mishale yao mikali, hivyo wanapaswa kubaki mbali. Ingawa zote zilikua na nia ya uhusiano wa karibu wakusaidiana, hii huenda isifanyike, kwa sababu zisizoepukika.
 
Arthur Schopenhauer alitumia fumbo hili kuelezea dhana yake kuhusu hali ya mtu binafsi katika uhusiano wa ujamii na wengine. Utata wa nungunungu huonyesha kwamba ingawa nia njema, umoja na urafiki wa kibinadamu hauwezi fanyika bila kiasi fulani cha kuumizana, na huongoza watu kwa  tabia za kujitahadhari na husiano hafifu. Utata wa nungunungu, unapendekeza kuwa mpole na kutumia wastani katika uhusiano na wengine ili kujichunga, na pia kama njia ya kuzingatia wengine. Utata wa nungunungu umetumiwa na mwanasiakologia Sigmund Freud kueleza upweke na dhana za kujitenga.
 
Fumbo hii ilitoka kwa ''Parerga und Paralipomena'', Volume II, Sura ya XXXI, Sehemu ya 396
 
Nungunugu kadhaa walikaribiana pamoja kutafuta joto katika siku ya baridi; lakini, vile walianza kuchomana na mishale yao, walilazimika kutawanyika. Lakini baridi iliwafukuza na kuwaleta tena pamoja, ambapo jambo lile lile lilifanyika tena. Hatimaye, baada ya mizunguko mingi ya kusogeana na kutawanyika, waligundua ni heri kubakisha nafasi kiasi kati yao. Kwa njia sawa, mahitaji hufanya nungunungu za kibinadamu kuletwa pamoja kwa ujamii, lakini hujipata wakisukumana na kuchomana na pembe za sifa mingi tofauti zinazopingana ambazo ziko kwa asili yao. Umbali wa wastani ambao hatimaye wanagundua ndio hali wanayoezaishi nayo, ni kanuni za upole na tabia mzuri; na wale wanopita mpaka huu wanaambiwa –kwa kiingereza- “keep your distance”. Kwa mpango huu mahitaji ya joto inatoshelezwa wastani tu; lakini pia watu hawadungwi. Mtu ambaye akona joto ndani yake anapendelea kubaki inje, ambapo hatadunga mtu wala hata dungwa yeye mwenyewe.
 
{{DEFAULTSORT:Schopenhauer, Arthur}}