Globu ya nyota : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Picha:A Large Persian Brass Celestial Globe with an ascription to Hadi Isfahani.jpg|thumb|Globu ya nyota ya Kiajemi ya karne ya 18, inaonyesha picha ya [[Hawa...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 20:29, 8 Oktoba 2017

Globu ya nyota (ing. celestial globe) ni tufe inayoonyesha michoro ya nyota na kundinyota usoni wake. Kwa hiyo ni kama ramani ya nyota iliyochorwa juu ya tufe au globu.

Globu ya nyota ya Kiajemi ya karne ya 18, inaonyesha picha ya Hawaa (Ophiuchus)
Atlasi akibeba globu ya nyota (Globu ya Farnese) ikionyesha kundinyota za Kantarusi (Centaurus) na Shuja (Hydra)

Ramani za aina hii zilitengenezwa tangu zamani na mfano wa kale iliyohifadhiwa ni globu ya Farnese ya karne ya 2 BK inayomwonyesha shujaa Atlasi anayebeba globu ya nyota kama ishara ya ulimwengu wote mbegani. Globu za aina hii zilikuwa kifaa muhimu cha mafundisho ya astronomia katika karne zilizopita.

Mtazamaji kwa kawaida anahitaji kuwaza ya kwamba yuko ndani ya tufe.