Kim Jong-un : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
 
Mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini lakini Vita baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili. Kila moja alianzisha serikali yake kulingana na itikadi yake. Warusi waliunga mkono utawala wa Kikomunisti Korea Kaskazini na Wamarekani waliunga mkono uchumi wa kibepari na serikali iliyochaguliwa kwa kura ya wengi Korea Kusini.
 
Kim alitangazwa kuwa kiongozi mkuu baada ya mazishi ya baba yake tarehe 28 Desemba 2011. Vyeo vyake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, Mwenyekiti wa Tume ya Mambo ya Ndani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea, na mwanachama wa Kamati ya Kudumu ya Politburo ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea. Mamo tarehe 9 Machi 2014, Kim Jong-un alichaguliwa bila kupingwa kuingia katika Bunge Kuu la Watu. Kim ana shahada mbili, moja ya [[fizikia]] kutoka [[Chuo Kikuu cha Kim Il-sung]], na nyigine kama afisa wa Jeshi katika Chuo Kikuu cha Jeshi cha Kim Il-sung.
 
Mnamo tarehe 12 Desemba 2013, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilitangaza kwamba kwa sababu ya "udanganyifu," aliamuru mauaji ya mjomba wake [[Jang Song-thaek]]. Kim Jong-un anaaminika kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya kaka yake, [[Kim Jong-nam]] nchini Malaysia mwezi Februari 2017.