Mjusi (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|400px|Nyota za kundinyota Mjusi (Lacerta ) katika sehemu yao ya angani File: Lacerta Hevelius.jpg|thumb|right|400px|Mju...'
 
Mstari 12:
Kundinyota hii haikujulikana kwa mabaharia Waswahili wa Kale wala kwa Waarabu au Wagiriki kwa sababu nyota zake ni hafifu sana. Katika enzi ya kale nyota hizi hazikupangwa kuwa sehemu ya kundinyota maalumu. Mjusi ni kati ya kundinyota zilizoanzishwa na mwanaastronomia [[Johannes Hevelius]] wa [[Danzig]] (Gdansk) mnamo mwaka [[1690]] BK. Akiwa mpika pombe na mfanyabiashara tajiri aliyeshika kwa muda pia umeya wa mji wake alikuwa hasa maarufu kwa kuangalia, kupima na kuorodhesha nyota pamoja na mke wake [[Elisabeth Hevelius]].
 
Hevelius aliyelenga kujaza mapengo kati ya kundinyota akiandika kwa Kilatini alichagua jina “Lacerta sive Stellio ” ([[Mjusi]] au [[Salamanda]]) lakini jina la pili halikutumiwa baadaye.
 
Lacerta - Mjusi imepokelewa kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na [[Umoja wa kimataifa wa astronomia]] kwa jina la Lacerta. Kifupi chake rasmi kufuatana na [[Ukia]] ni 'Lac'.<ref>[https://www.iau.org/public/themes/constellations/ The constellations], tovuti ya [[Ukia]], iliangaliwa Oktoba 2017</ref>