Kaunti ya Kiambu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Kuongeza infobox
Nimeongeza habari kuihusu kaunti.
Mstari 33:
 
 
'''Kaunti ya Kiambu''' ni mojawapo ya [[kaunti za Kenya]] zilizopo baada ya [[katiba mpya]] ya [[Jamhuri ya Kenya]] kupatikana [[mwaka]] [[2010]]. Ilikuwa mojawapo wa wilaya za Kenya katika Mkoa wa Kati baada ya nchi kupata uhuru. Mji mkuu wa kaunti hii ni mji wa [[Kiambu]].
Kaunti hii imepakana na kaunti za [[Kaunti ya Nairobi |Nairobi]] (kusini), [[Kaunti ya Machakos|Machakos]] (mashariki), [[Kaunti ya Nakuru|Nakuru]] (magharibi), [[Kaunti ya Nyandarua|Nyandarua]] (kaskazini magharibi) na [[Kaunti ya Murang'a|Murang'a]] (kaskazini). Kupakana na [[Nairobi]] kumeifanya iwe na idadi ya wakazi wengi mijini, kwa sababu ya maendeleo katika sekta ya mali yasiyohamishika. Sekta za viwanda na ukulima pia zimechangia kukuza kaunti hii kiuchumi.
 
==Serikali na Utawala==
[[Makao makuu]] yako [[Kiambu]].
===Utendaji===
Gavana, sasa Ferdinand Waititu, ndiye mkuu wa kaunti na serikali. Yeye huchaguliwa kwa muhula wa miaka mitano katika uchaguzi mkuu. Ana nguvu za utendaji na za kuteua wanakamati wa Kamati ya Utendaji ya Kaunti baada ya kuidhinishwa na Bunge la Kaunti. Hata ingawa mji mkuu wa kaunti uko [[Kiambu]], utendaji wa serikali uko mji wa [[Thika]].
 
===Bunge===
Bunge la Kaunti ya Kiambu ni lenye chumba kimoja. Lina wajumbe 60 waliochaguliwa kutoka wadi sitini za kaunti na wajumbe 27 walioteuliwa<ref> http://kiambucountyassembly.go.ke/assembly/about-us.html</ref>. Kila mjumbe anashikilia hatamu ya miaka mitano, inayofanywa upya katika uchaguzi mkuu. Spika wa bunge na naibu wake huchaguliwa na wajumbe. Bunge la Kiambu liko katika mji wa Kiambu.
 
===Mahakama===
Kuna Mahakama Muu ya Kiambu iliyoanzishwa Juni 20, 2016. Ina jaji mmoja.<ref> http://www.judiciary.go.ke/portal/blog/post/kiambu-gets-high-court</ref>
 
===Utawala===
Kamishna wa kaunti huteuliwa na Rais wa Kenya. Yeye ni mwakilishi wa rais kusaidia na mambo ya utawala wa serikali ya kitaifa.
 
{{mbegu-jio-KE}}
 
[[Jamii:Kaunti za Kenya]]