Paralaksi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Picha:Paralaksi mfano.png|300px|thumb|Mfano wa paralaksi: kutegemeana na mahali pa mtazamaji kiolwa kinachotazamiwa kitaonekana mbele ya sehemu ya buluu au ya...'
 
No edit summary
Mstari 15:
 
Paralaksi itakuwa kubwa zaidi kadri mstari wa msingi ni ndefu na nukta ya tatu (kiolwa cha kutazamiwa) iko karibu. Vilevile kinyume: kama nukta ya tatu iko mbali na mstari wa msingi si kubwa basi paralaksi huwa ndogo.
[[Picha:ParallaxeV2.png|300px|thumb|Paralaksi inasababisha nyota (njano) kuonekana mahali tofauti ikipimwa kutoka sehemu mbili tofauti za obiti ya Dunia]]
 
==Matumizi ya paralaksi kwa kukadiria umbali wa kiolwa==
Kama umbali kati ya nukta za mstari wa msingi unajulikana na pembe kwa nukta ya tatu linaweza kupimwa inawezekana kukadiria umbali wake kwa uhakika mkubwa. Mbinu huu unatumiwa katika [[fokasi]] ya [[kamera]] au vifaa vya upimaji ardhi na katika [[astronomia]].
 
==Paralaksi katika astronomia==
[[Picha:Paralaksi.png|thumb|300px|Namna ya kupima paralaksi ya nyota]]
Upimaji wa paralaksi ni msingi wa kujua umbali kutoka Dunia hadi [[sayari]] na nyota.
 
Paralaksi inatambuliwa kirahisi kwa umbali wa [[Mwezi (gimba la angani)|Mwezi]]. Mwezi unaonekana mbele ya nyota tofauti ukiangaliwa kutoka Afrika Kusini na kutoka Ulaya. Hii ni pia sababu ya kwamba [[kupatwa kwa Jua]] kunaonekana tofauti kwenye sehemu mbalimbali za Dunia. Kama Jua linapatwa kisehemu tu pale tulipo tukio hilohilo linaweza kuonekana kama kupatwa kabisa kwenye sehemu kusini au kaskazini zaidi kutoka kwetu.
 
Paralaksi ya sayari kama [[Zuhura]] itakuwa ndogo zaidi kwa sababu sayari hii iko mbali zaidi hivyo tofauti mbele za nyota nyuma yake ni kiasi tu ikitazamiwa kutoka sehemu tofauti za Dunia. [[Mpito wa Zuhura]] mbele ya [[Jua]] ulileta nafasi ya kupima paralaksi linganifu na kona ya Jua na hivyo kuwa msingi kwa makadirio ya kwanza kwa ajili ya kujua [[kizio astronomia]]. Hapa kipenyo cha Dunia kinachojulikana kilikuwa kiasi cha mstari wa msingi.
 
Kwa kupima umbali wa nyota nusukipenyo cha [[obiti]] ya Dunia ni mstari wa msingi. Paralaksi ni pembe kati ya mstari wa nusukipenyo hii na nyota inayotazamiwa. Kama paralaksi hii inalingana na [[sekunde ya tao|sekunde moja ya tao]] yaani sehemu ya 1/3600 ya nyuzi moja basi umbali wake ni kilomita bilioni 31 au miaka ya nuru 3.26. Umbali huu huitwa pia kama [[parsek]] moja na hii ni kiwango kinachotumiwa mara nyingi na wanaastronomia kutaja umbali wake.
 
Paralaksi ya nyota ni ndogo hivyo haikutambuliwa kwa muda mrefu. Mara ya kwanza alifaulu Mjerumani Friedrich Wilhelm Bessel mwaka 1838 kupima mabadiliko ya nyota [[Dajaja (kundinyota)|61 Cygni]] kwa kulinganisha vipimo mbalimbali alizofanya kila baada ya nusu mwaka. Alifikia 0.31" na kiwango kinachofikiwa leo kwa vifaa bora ni 0.29" kinacholingana na miaka ya nuru 11.
 
Kwa nyota za mbali ni vigumu zaidi kufikia vipimo kamili. Chombo cha angani [[Hipparcos]] (''High Precision Parallax Collecting Satellite'') cha taasisi ya [[ESA]] kilichorushwa kwenye anga la nje mwaka 1989 kiliweza kuleta vipimo vipya kwa nyota 118,000. Tangu mwaka 2013 chombo cha [[Gaia (chombo cha angani)|Gaia]] kinaendelea na vipimo vya bilioni 1 ya nyota.
 
==Marejeo==
* {{Cite book | last=Hirshfeld | first=Alan w. |title=Parallax: The Race to Measure the Cosmos |location=New York|publisher = W. H. Freeman |date=2001 |isbn = 0-7167-3711-6 | ref=harv | postscript=<!--None-->}}
* {{Cite book | last=Whipple | first=Fred L. | date=2007 | title=Earth Moon and Planets | isbn=1-4067-6413-2 | publisher=Read Books | ref=harv | postscript=<!--None--> }}.
* {{Cite book | last=Zeilik | first=Michael A. | last2=Gregory | first2=Stephan A. | title=Introductory Astronomy & Astrophysics | edition=4th | date=1998 | publisher=Saunders College Publishing | isbn=0-03-006228-4 | ref=harv | postscript=<!--None--> }}.
 
== Viungo vya Nje ==
* [http://inner.geek.nz/javascript/parallax/ Instructions for having background images on a web page use parallax effects]
* [http://www.perseus.gr/Astro-Lunar-Parallax.htm Actual parallax project measuring the distance to the moon within 2.3%]
* BBC's [http://www.bbc.co.uk/science/space/universe/questions_and_ideas/astronomical_distances/#p00bf0l7 Sky at Night] programme: Patrick Moore demonstrates Parallax using Cricket. (Requires [[RealPlayer]])
* Berkeley Center for Cosmological Physics [https://web.archive.org/web/20120303140550/http://bccp.lbl.gov/Academy/pdfs/Parallax.pdf Parallax]
* [http://www.phy6.org/stargaze/Sparalax.htm Parallax] on an educational website, including a quick estimate of distance based on parallax using eyes and a thumb only