William Herschel : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '300px|thumb|Wilhelm - William Herschel mnamo mwaka 1785 Picha:Sir William Herschel and Caroline Herschel. Wellcome V0002731 (...'
 
No edit summary
Mstari 3:
'''Friedrich Wilhelm Herschel''' (kwa Kiingereza: '''Frederick William''', [[15 Novemba]] [[1738]] – [[25 Agosti]] [[1822]]) alikuwa mtungaji wa muziki na mwanaastronomia kutoka nchini [[Ujerumani]] aliyeishi na kufanikiwa [[Uingereza]].
 
Alipata umaarufu hasa kama mgunduzi wa [[sayari]] ya [[Uranus]]. Kasoko moja kwenye [[Mwezi]] ilipewa jina la Kasoko ya Herschel kwa heshima ya michango wake, pamoja na kasoko kwenye [[Mirihi]] na kwenye mwezi [[Mimas]] wa [[Zohali]].
 
==Maisha==
Herschel alizaliwa katika familia ya Walutheri katika utemi wa Hannover kwenye kaskazini ya Ujerumani<ref>leo katika [[Saksonia Chini|Jimbo la Saksonia Chini]]</ref>. Familia ilikuwa ya asili ya Kiyahudi kutoka [[Moravia]]. Babake alikuwa mwanamuziki katika bendi la jeshi la mtemi. Wakati ule watemi wa Hannover walikuwa pia wafalme wa Uingereza. Wilhelm alimfuata baba kama mpiga filimbi wa [[oboe]] na [[fidla]] kattika bendi ya kijeshi. Kwa njia hii kijana Wilhelm alifika Uingereza kwa umri wa miaka 19 alipobaki na kuendelea kuishi.
 
Herschel aliendelea na kazi ya muziki akaendelea kuwa kiongozi wa bendi hadi kushika nafasi ya mkurugenzi wa muziki katika mji wa [[Bath]] alipoishi pamoja na dadayedadake Caroline. Alikuwa pia mpiga [[kinanda za filimbi]] kanisani. Alitunga muziki ya kiroho na ya burudani.
 
Tangu miaka ya 1770 alianza kushughulikia mambo ya hisabati alikovutwa kutokana na kazi ya kutunga muziki na kutafakari nadharia ya muziki. Kupitia rafiki mmoja alivutwa na astronomia. Alianza kutengeneza na kuuza vifaa vya darubini alizoweza kuboresha.