Muundo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
imeandikwa na athumani chipofya
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:55, 14 Januari 2018

Muundo ni mpangilio na mtiririko wa visa na matukio katika kazi ya kifasihi.Hapa tunachunguza jinsi msanii wa kazi hiyo alivyounda na alivyounganisha tukio moja na jingine,kitendo kimoja na kingine,sura moja na nyingine .Tunapohakiki muundo katika kazi ya kifasihi hasa riwaya na tamthilia.

  • kuna mambo ya kuzingatia.Mambo hayo ni,
  • Aina ya muundo
  • Mgawanyo wa kazi hiyo
  • umbo la kazi hiyo

Aina za muundo

  • kuna aina tatu za muundo,Aina hizo ni.

Muundo msago

  • Huu ni muundo wa moja kwa moja ambao visa na matukio vimepangwa katika hali ya kufuatana kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho.

Muundo rukia

  • Ni aina ya visa na matukio.Hapa kunakuwa na visa viwili au zaidi ambavyo hurukiana katika kusimuliwa kwake na mwisho wa visa hivi hugawana na kuwa kisa kimoja.

Muundo changamano

  • Huu ni muundo ambao kunakuwa na muundo wa msago na rukia.Hapa visa huanza kwa urejeshi na kumaliziwa na msago.

mgawanyo wa kazi hiyo

  • katika mgawanyo wa kazi mhakiki anapaswa kueleza
  • sura/namba=riwaya
  • sehemu/onesha=tamthiliya
  • Idadi ya mstari kwa ubeti =ushauri
  • ikumbukwe kwamba mwandishi anaweza kugawa kazi yake katika sehemu lakini akaipa picha sura na taswira.

Umbo la kazi hiyo

  • katikakuangalia umbo la kazi mhakiki anapaswa kueleza kama kazi hiyo,riwaya tamthiliya au ushairi.