Nyotamkia ya Halley : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 12:
 
==Tabia==
Wakati wa kupita karibu na Jua katika mwaka 1987 [[vipimaanga]] kadhaa vilirushwa juu na hasa [[kipimaanga]] ''[[Kipimaanga Giotto |kipimaanga Giotto]]'' kilifaulu kupata data nyingi. Kiini cha Halley kina ukubwa wa [[kilomita]] 15.3 × 7.2 × 7.2. Uso wake ni mweusimweusi na mwekundu kidogo. Kutoka upande wa uso uliotazama Jua kulikuwa na michirizi ya gesi na vumbi inayounda “mkia” wake. Mata ya michirizi hii ilikuwa hasa [[maji]] na [[monoksidi kabonia]], pamoja na [[methani]] na [[amonia]].
 
Mwili wa nyotamkia ni mchanganyiko wa mawe, vumbi na barafu. Ikifuata obiti yake na kukaribia jua kiasi cha kutosha inaanza kuonekana kama nyota ikiakisi nuru ya jua. Ikikaribia jua zaidi sehemu ya barafu yake inaanza kuyeyuka kuwa mvuke unaotoka kwenye kiini cha nyotamkia yenyewe na kuizungusha kama angahewa. Gesi hii inasukumwa na [[upepo wa Jua]] (shinikizo ya miale ya nuru itokanayo katika Jua) na kuonekana kama "mkia". Mkia huu unaelekea kila wakati upande usio wa jua kwa sababu upepo wa jua unasukuma mvuke upande ule.
 
 
== Mipito ya Nyotamkia wa Halley kwenye Periheli iliyorepotiwa==